Jumla ya mbao 1500 zimekamatwa wilayani Tanganyika mkoani katavi zikisafirishwa bila kibali kuelekea mkoani kigoma.
Mbao hizo zimekamatwa usiku wa kuamakia jana na askari wa jeshi la polisi waliokuwa doria katika mpaka wa wilaya ya tangayika na uvinza. Akizungumza mara baada ya kukamatwa kwa shehena hiyo mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando amesema kuwa watahakikisha wanapambana na kudhibiti uvunaji wa misitu kiholela kwa manufaa ya taifa.
Amesema mbao hizo zilikuwa shehena ya lori baada ya kuvunwa kwa mazao ya misitu bila kuwa na kibali kutoka idara ya maliasili.
Dc mhando ameongeza kuwa Shehena hiyo ilikuwa imepakiwa kwenye magari mawili aina ya Nissan disel yenye namba za usajili T 763 ANZ na T 561 BBT ambayo yametelekezwa na madereva baada ya kuwaona maafisa misitu huku mtu mmoja akikamatwa.
kwa upandea wake Afisa misitu wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Denis Sikamtoni amewataka raia kuendelea kushirikiana nao kwa kuwapatia taarifa ili wazianyie kazi na kuendelea kutunza maliasili ya nchi.
No comments:
Post a Comment