Advertisements

Saturday, October 22, 2016

MSAADA WA TETEMEKO KAGERA KUTOKA NORTHERN CALIFORNIA WAPOKELEWA KAGERA

JUMUIYA YA WATANZANIA NORTHERN CALIFORNIA YACHANGIA MAAFA KAGERA
(Tsh milioni 10,271,150/=)

Jumuiya ya watanzania na marafiki wa Northern California wametoa mchango wao wa kiasi cha Tsh milioni kumi laki mbili sabini na moja elfu na mia moja hamsini. (Tsh milioni 10,271,150/=) kusaidia serikali katika kukabiliana na wahanga pamoja na maafa yaliyotokana na tetemeko mkoani Kagera

Shukrani ziwaendee wote walioweka mkono wao na nguvu zao katika kufanikisha hili zoezi bila kusahau  chama cha watanzania eneo hili la ghuba (TCO) kwa kusaidia kuratibu zoezi zima na pia kuchangia kwa kiasi kikubwa.

Fedha zimetumwa katika account ya bank ya CRDB kama ilivyoelekezwa na serikali ili zifike katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera ambapo ndio shughuli zote za zoezi hili zinaratibiwa.
Katibu wa mkuu wa mkoa wa Kagera Thomas James Salala amethibitisha kiasi cha pesa hiyo kuingia katika account hiyo na kutoa shukrani kwa niaba ya mkuu wa mkoa. Tafadhali fungua ambatanisho kuhakikisha hilo.
Aksanteni sana.

Erick Byorwango- Muenezi.

No comments: