Advertisements

Wednesday, October 19, 2016

Mwanafunzi apigwa Dar, ‘afa, afufuka’ mochwari

Image result for Gilles Muroto
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto

By Pamela Chilongola, Mwananchi pchilongola@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Lumo wilayani Temeke, Isack Ernest alionja mauti baada ya kupigwa na wananchi kiasi cha kufikiriwa kwamba amekufa, akapelekwa chumba cha maiti ambako alizinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto alisema jana kwamba kijana huyo alipigwa hadi kupoteza fahamu na alipofikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke aliwekwa kwenye chumba cha maiti pamoja na kijana mwingine aliyeuawa katika tukio hilo.

“Mwanafunzi huyo hali akiwa amelazwa pamoja na maiti nyingine zinazosubiri kuwekwa katika majokofu, alitikisika kutokana na baridi ya chumba cha maiti, wahudumu wakamwona na kumtoa, wakamvalisha nguo za maiti nyingine, akarudishwa hospitalini kwa ajili ya huduma,” alifafanua Kamanda Muroto.

Habari zaidi soma Gazeti la Mwananchi

No comments: