ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 11, 2016

TANZANIA IMEANZA KUFANYA UTAFITI WA MBEGU YA MAHINDI MEUPE KWA KUTUMIA GMO

 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda, akizindua utafiti huo katika Kituo cha Utafiti cha Makutupora mkoani Dodoma juzi.
 Watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakiwa tayari kwa upandaji wa mbegu hizo katika Kituo cha Utafiti cha Makutopora mkoani Dodoma.
 Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi, akishiriki kupanda mbegu hizo.
Mkurugenzi wa Sayansi Hai wa Costech, Dk.Flora Tibazarwa akishiriki katika zoezi hilo la upandaji mbegu hizo.
Mshauri wa Mradi wa WEMA, Dk. Alois Kullaya  (kushoto) na Meneja mradi huo Mr  Silvester  wakishiriki kwenye upandaji wa mbegu hizo.
 Watafiti wakichoma masalia ya vifungashio vya mbegu za mahindi kama sheria ya GMO inavyoelekeza baada ya zoezi hilo.

Na Dotto Mwaibale
KWA mara ya kwanza Tanzania  imeanza kufanya utafiti wa mbegu ya mahindi meupe kwa kutumia teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) ambao utachukua takriban miaka mitatu ili kupata matokeo ya mbegu nzuri itakayostahimili mabadiliko ya hali ya hewa ambayo imekuwa changamoto kubwa kwa wakulima.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Hassan Mshinda alisema kuanza kwa utafiti huo ni hatua nzuri kwa nchi katika kuinua kilimo nchini.

Alisema utafiti huo ambao unafanyika katika nchi tano za Afrika, kwa hapa nchini unafanyika katika kituo cha Makutopora mkoani Dodoma na kuwa nchi hizo  nyingine ni Kenya, Uganda, Africa ya Kusini na Msumbiji. 

Mtafiti na Mshauri wa mradi wa mahindi yanayostahimili ukame ( WEMA) Dk. Alois Kullaya, alisema Tanzania ilikuwa ikifanya tafiti katika hatua ya maabara, na sasa kwa mara ya kwanza wapanda kwenye mazingira halisia. " Ni kweli tarehe tano ya mwezi huu, tulipanda mahindi meupe katika hatua ya utafiti kwenye mazingira. Tunataka tujiridhishe na uwezo wa mahindi hayo katika kustahimili ukame". Matokeo ya utafiti huu, utatoa nafasi kwetu kama watafiti na viongozi wetu kufanya maamuzi yenye tija kwa taifa badala ya kuwa watazamaji na kushambikia marumbano tusiyofahamu chanzo chake" alisema Kullaya.

Mtafiti Kiongozi wa masuala ya bioteknolojia kutoka Costech Dk. Nicholas Nyange aliishukuru serikali kwa kuruhusu watafiti wake kuweza kufanya majaribio ya uhandisi jeni hapa nchi. Hii ni hatua nzuri katika nchi yoyote inayoamini katika maendeleo ya sayansi na teknolojia. 
"Tumekuwa tukitishiwa kama watoto  Usiguse GMO utakufa, wakati nchi nyingine wanazalisha nakufanya biashara. Tunafanya biashara kubwa na India, China, Marekani na Afrika ya Kusini, na hawa wote wanatumia teknolojia ya uhandisi jeni". 

 "Tufanye utafiti, tuone kama tutakufa kweli au tutatoka kimasomaso"  aliongeza Nyange kwa tabasamu. 

Itakumbukwa kuwa Mradi wa WEMA hadi sasa  umezalisha mbegu 11 za mahindi kwa njia za kawaida. Na baadhi ya mbegu hizo zimeingia sokoni mwaka huu kwa bei ya kawaida. Hivyo, uzalishaji wa Mahindi ya GMO itakuwa ni hatua mbele katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi. 

5 comments:

Anonymous said...

Hiyo ni hatari kwani huo mfumo ni wa kuogopwa kama ukoma. Ni chanzo cha kuua mbegu zetu za asili na kuwa watunwa wa kutegemea mfumo wa mbegu unaomilikiwa na mabepari. Yaani ni hatari sana na usilolijua ni usiku wa kiza na Africa ipo hatarini kupoteza uasili wa mbegu zake. Waafrica tumekuwa watumwa katika mfumo wa biashara duniani pamoja na mfumo wa fedha na sasa tunakuwa watumwa ya jinsi gani tuoteshe mazao yetu.Kwanini hapa Marekani na nchi zilizoendelea bidhaa zote bora na salama kwa mlaji zinaalama au lebo zinazosema(NOON GTMO)? Nafikiri ingekuwa busara Serikali na taasisi husika wangefanya utafiti kwanini nchi zilizoingia katika mfumo huo zinajuta? Ni maoni tu na wala sina usiasa katika hili bali ni uzalendo wa nchi yangu.

Anonymous said...

Siku zote nchi zetu za kiaafrika hukurupuka ku comply na programs wanazosogezewa na western countries bila kufanya deep analysis ya impact zake.pamoja na hili GMO kuna issue kama za kupiga marufuku matumizi ya plastics.Nchi zilizoendelea ambao ndio watuamiaji wakubwa wa plastics wame impose taxes na kuincourage recycling projects ili kulinda ajira na kuongea kipato waaafrica kama kawaida yetu tumetangaza total ban with unemployment rates zikininginia at over 12% na uchumi unaishi ICU.

Anonymous said...

Umeongea vizuri sana ndugu yangu hapo juu. Hizo mbegu ni hatari na ni za kuziogopa sana.

Unknown said...

Namwuunga mkono huyu mwandishi hapa juu. Please view a movie King Corn. Inahusu mbegu ya mahindi yaliyotumika na kuleta madhara kwa binadamu. (Obesity) Hata ikatumika kwa ngombe. Binadamu wakala nyama ya hao ngombe ikawaletea madhara makubwa ya afya. Jamaani tuheshimu mababu zetu walivyotulea na kutukuza with organic vyakula na mbegu asilia. Tujaribu kutafuta namna ya kuboresha ardhi na rutuba.

Anonymous said...

TUMEKWISHA NAONA HAO JAMAA WA COSTECH WAKIFURAHIA KIFO CHA SUMU YA GMO HEBU WAUULIZE NCHI ZA CANADA NA INDIA PAMOJA NA BRAZIL KWA NINI KUNA UGONJWA WA ZIKA? UMETOKAKANA NA HIZO SUMU ZA GMO.