Advertisements

Wednesday, October 19, 2016

YALIYOJIRI KATIKA KONGAMANO LA WAWAKILISHI WA WANAWAKE KUTOKA AFRIKA WALIOKUTANA KUJADILI MADAI YAO YA UMILIKI WA ARDHI

Wawakilishi wa Wanawake kutoka nchini Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja  wakati wa kuwapokea wanawake waliopanda mlima Kilimanjaro na kusimika madai yao juu ya umiliki wa Ardhi.
Wawakilishi wa wanawake wa Uganda  wakiwasubilia wanawake wenzao waliopanda mlima Kilimanjaro.

Wawakilishi wa wanawake kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakiimba nyimbo mbalimbali walipokuwa wanaelekea eneo la Marangu lilipo geiti la kupandia mlima Kilimanjaro ili kuwapongeza wanawake waliopanda mlima kilimanjaro na kufika katika kilele cha mlima huo na kuweka madai yao hapo.
Wawakilishi wa wanawake kutoka nchini Tanzania wakiwapokea wanawake wawili waliofanikiwa kufika kilele cha mlima Kilimanjaro na kuweka Madai ya hasa la mwanamke kupata haki sawa katika kumiliki Ardhi
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi akimpongeza Tatu Maleta(aliyekaa) aliyefanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro na kuweza kuweka madai ya kupata haki ya kumiliki ardhi.Aliyekaa upande wa kulia ni  Bi. Flora Matiasi aliyefanikiwa kufika katika kilele cha mlima Kilimanjaro.
Wanawake wa Kitanzania waliofanikiwa kufika kilele cha mlima Kilimanjaro wakiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa wanawake wa Tanzania
Wanawake wa Kitanzania wakiwa wanajiandaa kuingia ukumbini kwa ajili ya kufunga kongamano lililowakutanisha wawakilishi wa wanawake wa Afrika waliokutana katika Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.
Wawakilishi wa wanawake kutoka nchini Nigeria wakiingia ukumbini wakati wa kufunga kongamano lililowakutanisha wawakilishi wa wanawake wa Afrika  uliofanyika katika Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.
Wawakilishi wa wanawake kutoka nchini Malawi wakiingia ukumbini wakati wa kufunga kongamano lililowakutanisha wawakilishi wa wanawake wa Afrika  uliofanyika katika Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.
Wawakilishi wa wanawake kutoka nchini Uganda wakicheza kwa firaha wakati wa kuingia ukumbini wakati wa kufunga kongamano lililowakutanisha wawakilishi wa wanawake wa Afrika  uliofanyika katika Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi akiwaongoza wawakilishi wa wanawake kutoka nchini Tanzania wakati walipokuwa wakiingia ukumbini kwa ajili ya ufungajiwa kongamano lililowakutanisha wawakilishi wa wanawake wa Afrika uliofanyika katika Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.
Wawakilishi wa wanawake kutoka nchini Tanzania wakiserebuka kwa furaha
Baadhi ya wanawake kutoka barani Afrika waliokutana katika ukumbi wa Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha

Mwanamziki na Mwanaharakati wa Haki za wanawake, Sister D kutoka nchini Zambia akitoa burudani wakati wa kufunga kongamano lililowakutanisha wawakilishi wa wanawake kutoka nchini mbalimbali barani Afrika  uliofanyika katika Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.
Mwanamziki na Mwanaharakati wa Haki za wanawake, Michael kutoka nchini Zambia akitumbuiza wakati wa kufunga kongamano lililowakutanisha wawakilishi wa wanawake kutoka nchini mbalimbali baran Afrika.
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Dkt. Vincensia Shale akizungumza jambo wakati wa kufunga kongamano hilo
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi(kushoto)akifuatilia kongamano
Maneja wa Programu ya Ushawishi na Utetezi, Grace Kisetu(aliyeshika kipaza sauti) akisoma  wasifu wa viongozi waliopewa tuzo za mchango wao katika kupigania haki ya wanawake.
Mratibu wa Kituo cha usuluishi cha TAMWA, Bi. Gladness Hemedi Munuo akipokea tuzo kwa niaba ya Thabisa Siwale ambaye ilipigania haki ya wanawake kupata ardhi kwenye ukumbi wa  Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.
Mke wa Marehemu Saidi Augustino akipokea tuzo ya mume wake aliyekuwa jaji na kuwapiania wnawake kupata haki zao katika jamii kwenye ukumbi wa  Chuo cha MS-TCDC mkoani Arusha.

No comments: