Advertisements

Thursday, November 10, 2016

Alichokiandika Alikiba baada ya MTV EMA kumtangaza Best African Act 2016


November 9 2016 ndio siku ambayo taarifa za waandaaji wa tuzo za MTV EMAwalimtumia taarifa Alikiba kupitia menejiment yake kuwa ni mshindi wa tuzo ya Best African Act na kuwa ilitolewa kwa Wizkid wa Nigeria kimakosa ila yeye ndio alistahili kuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka 2016.
Siku moja baada ya MTV EMA kumfikishia taarifa hizo na leo November 10 kuzitangaza rasmi kupitia mitandao yao ya kijamii, Alikiba ametumia ukurasa wake wa instagram kuwashukuru mashabiki wake, vyombo vya habari na wote wanaomuunga pamoja na waandaaji wa tuzo hizo.

“Namshukuru MUNGU Na Shukrani kwa MTV kwa heshima hii, nina furaha sana kwa ushindi huu, ni heshima kwangu na nchi yangu Tanzania pamoja na East Africa nzima kiujumla. Shukrani sana kwa familia yangu, management yangu na mashabiki zangu wote – nawapenda sana#bloodfanswaalikiba #Kajiandae#KingKiba

No comments: