Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Abdallah Kilima akizungumza na Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Yahel Vilan ambaye alitembelea Wizarani leo. Mazungumzo yao yalijikita katika masuala ya ushirikiano wa kidiplomasia katika maeneo mbalimbali yakiwemo miradi ya maendendeleo hususan katika sekta za afya,elimu, biashara, kilimo na Ulinzi.
Mhe. Vilan akizungumza ambapo alieleza kuwa Israel itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kuwa inatekeleza azma ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Wakiwa katika picha ya pamoja.
Mazungumzo yakiendelea.
No comments:
Post a Comment