ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 25, 2016

DK. KIGWANGALLA ATUNUKU VYETI WAITIMU SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU

 Na Anthony Ishengoma
Serikali inajipanga kuajili wataalamu wa maendeleo ya jamii 5,554 kwa kipindi cha miaka mitano ili waweze kutoa huduma za maendeleo ya jamii kuanzia  ngazi ya Serikali kuu hadi kijiji kama ilivyokuwa kwa utawala wa amu ya kwanza nchini.
Akihutubia wakati wa Mahafari ya sita ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tenguru nje kidogo ya jiji  la Arusha Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Hamis Kigwangalla amesema serikali ya awamu ya kwanza ilikuwa na idadi kubwa ya mabibi na mabwana maendeleo ya jamii kila kata.
 Aliongeza kuwa kwasasa wataalamu katika sekta ya maendeleo ya jamii  wameanza kupungua sana na kukitaka chuo kuongeza udaili wa wanafunzi ili kuendana na azima ya serikali ya kuwa na wataalamu awa kila wilaya na kata.
Aidha aliitaka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kuendela kutoa taaluma yenye viwango na  bora na uzingatiwe katika mchakato wote wa utoaji mafunzo kuanzia kwenye udahili wa wanafunzi wenye sifa na vigezo ili kujenga jamii ya wasomi wenye tija katika Taifa letu.
  Alisema Nchi itabadilika sana na kuwa na maendeleo ikiwa wanataaluma wa Nchi hii wataipenda Nchi yao kama ambavyo kila mtu ampendavyo mama yake nakujituma sana katika utendaji kazi utaendana na falsafa ya hapa kazi tu.
Naye Mkuu wa Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Anatory Bunduki wakati akuhutubia Mahafari hayo amesema kuwa pamoja na mikakati iliyopo ya kuboresha chuo hicho kwasasa chuo kimeanzisha kituo cha taifa cha utafiti na uhifadhi wa machapisho ya wanawake Nchini kituo ambacho kimeanzishwa kwa ushirikiano wa UNESCO na UNFPA pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Mkuu wa chuo alienedelea kusema lengo la kuanzishwa kwa kutuo hicho ni kufanya tafiti za kina kwa masuala ya wanawake, jinsia, watoto wa kike ili kuwainua kiuchumi, kisiasa,kiutamaduni na kijamii na kuzitumia tafiti hizi kujadili katika kuandaa sera na kutoa maamuzi yanayojumuisha amsuala ya kijinsia katika kutekeleza sera mbalimbali hapa Nchini.


Mahafaria ya sita ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru yametoa wahitimu katika fani za astashahada, shahada ya kwanza na stashahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii.

No comments: