Advertisements

Friday, November 11, 2016

Lema afikishwa mahakamani

By Emmanuel Herman, Mwananchi eherman@mwananchi.co.tz

Arusha. Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Lema anayekabiliwa na tuhuma za uchochezi amefikishwa mahakamani hapo kwa mapema leo (Ijumaa) asubuhi akiwa na watuhumiwa wengine na kupelekwa moja kwa moja mahabusu akisubiri uamuzi wa mahakama wa kupewa dhamana au la.

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema) Joshua Nassari amesema afya ya mbunge huyo ni njema na wanasubiri mahakama ifanye uamuzi wake hapo mchana.

Kuhusu usalama Jeshi la polisi limeimarisha usalama ndani na nje ya mahakama hiyo huku wafuasi wa Chadema wakiwa katika mahakama hiyo wakisubiri hatma ya kiongozi wao.

No comments: