Advertisements

Saturday, November 19, 2016

Lukuvi akabidhi polisi majina 30 ya matapeli wa ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
By Tumaini Msowoya, Mwananchi tmsowoya@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amekabidhi polisi majina ya watu 30 wanaodaiwa kuwa matapeli wa ardhi ili washughulikiwe.

Waziri huyo amelidokeza gazeti hili kuwa amekabidhi majina hayo kwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro ambaye alithibitisha kupokea majina hayo na kwamba tayari yameshafunguliwa majalada kwa ajili ya upelelezi.

“Ni mapema mno kuzungumzia jambo hili, kwa sababu lipo kwa wapelelezi. Ni kweli majina haya tumeyapokea na tayari majalada yamefunguliwa,” alisema.

No comments: