Advertisements

Sunday, November 20, 2016

MISA YA KISWAHILI NEW YORK LEO JUMAPILI

Image result for 120 East 106 Street, New York, NY 10029
Wakristu wapendwa,
Tumsifu Yesu Kristu.
Padre Peter Mushi na Padre Godfrey Amobi, wanapenda kuwatangazia ya kuwa,
Misa yetu ya kiswahili itafanyika Jumapili, tarehe 20 Mwezi Novemba, 2016, Saa 8:00 mchana (Sunday 20 November, 2016 at 2 pm). Tunawakaribisha wakristu wote watanzania na Afrika ya Mashariki wajiunge nasi katika Misa hii.
Pamoja na watu wote wanaopenda kuhudhuria ibada ya Kiswahili.


Anwani yetu ni: Kanisa la Mt. Cecilia, 120 East 106 Street, New York, NY 10029. Between Lexington and Park Avenue.


Chukua Train # 6. Mpaka kituo cha 110 St. Halafu tembea ukirudi mpaka 106 St.


Ni matumaini yetu kwamba mtafika kwa wingi. Karibuni tumtukuze Muumba Wetu kwa lugha yetu ya Kiswahili.
Mbarikiwe. Kutoka kwa Padre Peter Mushi na Padre Godfrey Amobi


Karibuni...

No comments: