Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa
anatoka kwenye Wodi ya Sewahaji katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kurejea nyumbani mara baada ya kuruhusiwa baada ya kupata
nafuu. Mama Janeth Magufuli alikuwa amelazwa hospitalini hapo tangu tarehe 9
Novemba 2016.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Raymond Mwenesano, Mkuu wa Idara
ya Wagonjwa wa nje na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurejea
nyumbani baada ya kupata nafuu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru
Dkt. Edward Ngwalle, Daktari wa Rais mara baada ya kuruhusiwa kutoka
hospitalini hapo na kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru
Dkt. Benard Kepha ambaye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura na ajali katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka na kurejea
nyumbani mara baada ya kupata nafuu. Picha
na IKULU
3 comments:
Hii ajabu kweli kweli. huyu mama kulazwa na kutibiwa nchini kama walalahoi wengine? Kweli nchi inaweza kubadilika. tunamwombea kupona na kuwashukuru madaktari wetu nchini kwa kazi nzuri.
Kama mama yetu mke wa RAISI anatibiwa Mhimbili, ni kwanini viongozi wengine wa taifa wanapelekwa nje ya nchi kwa matibabu?????
Ina tegemea naugonjwa aliokuwa anaumwa...Ingawaje na mpongeza pia kwa kukubali kutibiwa muhimbili maana wapo wake wa wakubwa hata kichwa kikiuma anaenda Nje
Post a Comment