Advertisements

Friday, November 11, 2016

MSIBA WA MZEE WETU SAMWEL SITTA DMV

Image result for samwel sitta
Kwanza tunapenda kuwashukuru mno kwa kutufariji katika msiba wa baba yetu mzee Samwel Sitta uliotokea Ujerumani alipokua ameenda kwa matibabu.

Pia tunatoa shukurani nyingi kwa msaada wenu wa hali na mali mlioutoa katika kipindi hiki cha msiba wa mpendwa baba yetu.

Pia tungependa kuwataarifu kuwa wafiwa wamefanikiwa kwenda nyumbani kwa mazishi na kutokana na hilo kwa sasa shughuli za msiba hapa DMV zimesitishwa rasmi mpaka hapo tutakapotoa taarifa ya kurejea kutoka Tanzania kwa Mtoto wa marehemu.

Kamati ya msiba DMV inatoa shukurani sana kwa ushiriki wako kwa njia moja au nyingine na kuweza kumfariji John Sitta katika kipindi hiki cha msiba wa baba yake.

Hatuna cha zaidi ya kusema asante na kile ulichotoa tunamwomba Mwenyezi Mungu akuzidishie mara elfu.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe na kwake tutarejea.

No comments: