ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 24, 2016

MUFTI ZUBEIRY AWATAKA WAISLAMU KUTUMIA SIKU YA MAULID KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA

Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir.

Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeiry amewataka waislamu wote nchini siku ya Maulid kuitumia siku hiyo kufanya usafi na kupanda miti. Sikukuu hiyo itafanyika tarehe 11 mwezi wa 12 mwaka huu.
Hayo yamesema na Mufti huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amewataka waislamu wote kutumia siku hiyo kutenda mema.

“Nichukue fursa hii kuwataka waislamu wote nchini kwa kuonyesha kwa vitendo yale yote mazuri aliyotuletea kipenzi chetu Mtume Muhammad, kwa msingi huu basi kufurahia huko kuendane na kuiga na kuendeleza mafundisho yake Mtume Muhammad siku hiyo tuitumie kwa mema mengi kufanya kama kupanda miti, kufagia na kuimarisha mazingira na kufanya mengi ili kuonyesha namna na kumuiga Mtume wetu,” alisema Shekhe Zubeiry.
Sikukuu hiyo kitaifa itanyika mkoani Singida wilaya ya Iramba huku kauli mbiu ya Maulid mwaka huu ikiwa ni ‘Muislam jitambue badilika amani na usalama ndiyo maisha yetu.’

No comments: