Advertisements

Thursday, November 17, 2016

NIDA kuanza kutoa namba za utambulisho Desemba

Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuanzia Desemba mwaka huu mpaka Januari 2017 itaanza kutoa namba maalum za utambuzi kwa wananchi.

Mkakati huo umetangazwa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba alipokutana na uongozi na wafanyakazi wa NIDA, kwa lengo la kujadili mikakati mbalimbali ya kuboresha utendaji wa mamlaka hiyo.

Alisema tayari serikali imekamilisha kanzidata ya wananchi walizozipata kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC na kwamba, tayari taasisi zaidi ya 35 zimeanza kutumia taarifa za NIDA katika kufanya utambuzi wa wafanyakazi wao sawia na kupunguza usumbufu kwa wananchi kuhusu taarifa zinazowahusu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NIDA Bw. Andrew Massawe alisema kwa zoezi la awali lililofanyika nchi nzima tayari wamefanya uhakiki wa kuwatambua watumishi wa serikali takribani laki tano na elfu sitini na tano.

1 comment:

Anonymous said...

Yaani hapa mnaanza kuoanisha namba na kuwa nazo kwenye tume ya Uchaguzi ili muendelezo wa kuchakachua matokeo uendelee!! kwani ni isiwe vitambulisho vya kitaifa NIDA inahusi8ka moja kwa moja kuna sababu gani kuainisha na tume ya uchaguzi.
Kwa nini tume ya uchaguzi isiendelee na kuandikisha wapiga kura wanaofikia miaka 18 kuendelea na wale ambao walishindwa kujiandikisha kwa namna moja au nyingine! wafanyakazi wa tume wapo na wanalipwa mishahara minono kwa kazi gani wakati uchaguzi umeisha 2015. hawaboreshi daftari w3ali nini. Ofisi ifungwe hadi mwaka 2018 kuelekea uchaguzi basi. Ni Tanzania pekee vituko vya aina hii vinaendekezwa!!