ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 3, 2016

Njaa yawatoa UDSM vitandani usiku

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wanaoishi Hosteli ya Mabibo wamekusanyika usiku huu kwenye lango la kuingilia, huku wakiimba wakiwataka viongozi wa Serikali ya Wanafunzi UDSM (Daruso) kuja kusikiliza kilio chao.
Huku wakiimba nyimbo mbalimbali ikiwamo ‘Kama siyo juhudi zako Nyerere…nchi hii ingekuwa wapi’ na ule maarufu wa ‘Solidarity forever’, walidumu kwenye mkusanyiko huo takriban kwa saa mbili hadi saa 6.15 waliopoamua kuondoa baada ya viongozi wao kutofika.
Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa, baadhi ya wanafunzi walisema wanaishi maisha ya shida kutokana na kutolipwa fedha za kujikimu na kwamba, mateso hayo yamesababishwa UDSM, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Serikali na Bodi ya Mikopo.
Hatua hiyo ilisababisha magari mawili ya polisi yaliyosheheni askari kupiga kambi eneo hilo, lakini kiongozi wao alisema hiyo ni doria ya kawaida ikiwa ni sehemu ya majukumu yao.

CHANZO: MWANANCHI

No comments: