Advertisements

Thursday, November 10, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MZEE JOSEPH MUNGAI JIJINI DAR LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa  mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Novemba 10, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji mjane wa  marehemu baada ya kutoa heshima zake za mwisho kwa  mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Novemba 10, 2016
Rais Dkt. John Pombe Magufuli (wa nne kushoto), Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa (wa tatu kushoto), Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wa tatu kulia), Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (kushoto), Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete (kulia) pamoja na viongozi wengine wakifatilia wasifu wa Marehemu Mzee Mungai, uliokuwa ukisomwa na Mtoto wake Mkubwa, Jimmy Mungai.
 Sehemu ya familia ya aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika hafla ya kuuaga mwili wa marehemy katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 10, 2016. Picha na Ikulu

No comments: