Advertisements

Friday, November 18, 2016

TANZIA MAREKANI NA NYUMBANI TANZANIA:

UPDATES ZA MSIBA WA MAMA YAKE MZAZI DADA LUCY MWAIJIBE

Kama tulivyohabarishana hapo awali kuhusu msiba wa mama yake mzazi dada yetu Lucy ambao umetokea nyumbani Tanzania jana, dada yetu Lucy anatarajia kuondoka jumamosi hii( 11/19/2016) kuelekea nyumbani Tanzania kuhudhuria shughuli za mazishi ya mama yake mpendwa. Mazishi ya mama yake dada Lucy yanatarajiwa kufanyika siku ya jumatatu (11/21/2016).

Kama ilivyo mira na desturi zetu za kufarijiana mara mwanajumuiya mwenzetu anapopatwa na matatizo, tunaomba watakaoweza waungane naye dada yetu Lucy nyumbani kwake kumfariji siku ya Alhamisi na Ijumaa kabla ya safari yake. Dada Lucy anatutegemea kwa maombi na faraja zetu katika kipindi hiki ambacho hakina ujasiri.

ADDRESS:
529 Hawthorne Avenue, Newark, NJ, 07112

Kwa taarifa zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao;

Contacts:
Neema #914-473-4101
Nyagaly #347-475-4313

M/Mungu ametoa na M/Mungu ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amina

UONGOZI
NEW YORK TANZANIAN COMMUNITY

1 comment:

John Mbatta said...

Pole sana dada Lucy kwa kufiwa na mama yako kipenzi. Mwenyezi Mungu akupe faraja stahiki na ninakutakia safari njema.