Advertisements

Wednesday, November 9, 2016

Utafiti waanika kilio cha ugumu wa maisha



Rais John Magufuli
By Peter Elias, Mwananchi pelias@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watu 95 kati ya 100 hawaoni kama kuna unafuu wa gharama za maisha katika kipindi cha mwaka mmoja wa utawala wa Rais John Magufuli.

Utafiti kuhusu utendaji wa Rais Magufuli katika kipindi cha mwaka mmoja wa kuwapo madarakani unaonyesha kuwa ameshughulikia suala la gharama za maisha kwa asilimia 5.2.

Utafiti huo uliofanywa na infotrak Research and Consulting uliodhaminiwa na Mwananchi Communications Limited, umetumia sampuli ya watu 1,000 kutoka katika kandazai Kaskazini, Kusini, Pwani, Kati, Zanzibar na Kanda ya Ziwa.

Pia, utafiti huo umehusisha watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea kutoka katika mikoa 15 na kata 113 katika kanda hizo.

Utafiti huo umeonyesha kuwa Rais Magufuli hajafanya vizuri katika suala la kuwawezesha vijana na wanawake kwani waliohojiwa walimpa asilimia 2.1 katika suala la kuwapa nafasi vijana na asilimia 2.6 katika kuwapa nafasi wanawake.

Vilevile utafiti unaonyesha kuwa utawala wa Rais Magufuli katika kipindi cha mwaka mmoja haukufanya vizuri katika masuala ya madini asilimia 2.7, utalii asilimia 3.3, biashara asilimia 4.3 na katika upatikanaji wa huduma za maji safi na salama ambapo wahojiwa walisema kwamba amelishughulikia suala hilo kwa asilimia tano.

No comments: