Advertisements

Friday, November 11, 2016

VETA kuanzisha kozi ya Utalii wa Kitamaduni

 Mwalimu wa Ufundi Mitambo wa Chuo cha VETA Mikumi, Peris Shao, akizungumza na waandishi wa habari juu maendeleo ya chuo hicho katika utoaji wa mafunzo ya ufundi Stadi.
 Wanafunzi wakiwa katika karakana ya ufundi Mitambo wakiwa katika mafunzo ya vitendo katika Chuo cha Mikumi.
 Mwalimu wa uChuo cha VETA Mikumii, James Maungu akitoa maelezo kwa waandishi wa habari walipotembelea karakana ya ufundi huo.
Mwanafunzi wa mwaka wa mwisho wa Chuo cha VETA Mikumi wakiwa katika mafunnzo ya vitendo karakana ya ufundi wa Magari.

Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Elimu na mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) kupitia chuo cha VETA Mikumi inatarajia kuanzisha kozi ya utalii wa kitamaduni ili kuwafundisha watanzania tamaduni ,mila na desturi ili kuulinda utamaduni wetu ambao unaonekana kupotea kadri teknolojia inavyozidi kukua kila siku.
Akizungumza na waandishi wa habari walipotemebelea chuo hicho Cha VETA Mikumi, Mkuu wa chuo hicho Christopher Ayo amesema kuwa uamuzi  huo umetokana na sekta ya utalii kuendelea kukua  mwaka hadi mwaka huku jamii  ikionekana kusahahu uhasilia wa tamaduni mbalimbali za kitanzania .
Amesema utamaduni ukitumika ipasavyo unaweza kuchangia ukuaji wa sekta ya utalii pamoja na uchumi nchini kutokana na ukweli kwamba nchi nyingi duniani zimeweza kulinda utamaduni kuweza kukuza uchumi wao.
Amesema chuo VETA Mikumi kwa kushirikiana na Chuo cha NOVA Scotia Communinity College cha nchini Canada  kinaanda kozi  hiyo itakayowezesha watanzania kujifunza kwa undani kuhusu utamaduni wao  kama vile  ngoma, vyakula vya asili ,sanaaa na historia ya makabila mbalimbali.
Ayo amesema maandalizi ya kuanzisha kozi hiyo yapo kwenye hatua za mwisho na kwamba kuanzia Januari, 2017 masomo  yataanza kutolewa.
Aidha mkuu huyo amesema walimu watano watakaofundisha masomo hayo wameshaandaliwa na kupatiwa mafunzo nchini Canada jinsi ya kutumia technologia katika kufundisha na kuandaa mitaala.
Ayo amesema VETA Mikumi itaendelea kutoa mafunzo kwa jamii inayowazunguka katika kuwaandaa vijana katika soko la ajira kwa kujiajiri au kuajiriwa na kuweza kuendesha maisha yao na kuchangia pato la taifa.
Ametoa rai kwa vijana wa mikumi na maeneo ya mengine ya Mkoa wa Morogoro kuchangamkia fursa za mafunzo zilizopo chuoni hapo ili kuweza kuwa sehemu ya wataalam watakaohudumia viwanda vitakavyojengwa kutokana na serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuweka msisitizo wa kuhakikisha nchi inakuwa ya  viwanda.

No comments: