ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 4, 2016

WASANII KUTOKA NIGERIA KUNOGESHA FAINALI YA TAMASHA LA FIESTA 2016, KESHO VIWANJA VYA LEADERS JIJINI DAR ES SALAAM

 Msanii kutoka Nigeria, Yemi Alade (kushoto) , akisalimiana na msanii Snura Mushi alipokuwa amewasili ukumbi wa mikutano wa Kampuni ya Simu ya Tigo kuzungumza na wanahabari wakati akijitambulisha kwao  Dar es Salaam leo jioni, kuhusu uwepo wake kwenye hitimisho la Tamasha la Fiesta litakalofanyika kesho viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Tamasha la Fiesta, Sebastian Maganga (kulia), akizungumza wakati wa kuwatambulisha wasanii wa hapa nchini na kutoka Nigeria ambao watatoa burudani kesho katika viwanja vya Leaders.
 Msanii kutoka Nigeria, Yemi Alade (kulia) , akizungumza katika mkutano wa kujitambulisha kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo jioni, kuhusu uwepo wake kwenye hitimisho la Tamasha la Fiesta litakalofanyika kesho viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam. Kushoto ni msanii mwenzake, Tecnomile na katikati ni msanii Snura Mushi.
 Msanii Tecnomile (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Meneja Huduma wa Masoko wa Tigo, Olivier Prentout.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Picha zikipigwa na msanii Tecnomile.

Na Dotto Mwaibale



WASANII Yemi Alade na Tecnomile kutoka Nigeria kesho watapanda jukwaani na washindi 16 washindano la Tigo Fiesta 

Super Nyota katika fainali ya Tamasha la Fiesta 2016 lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.


Wasanii hao wanatarajiwa kutoa burudani na nguvu katika viwanja hivyo itakayokwenda sanjari na kumpata mshindi wa tamasha hilo kwa mwaka 2016.



Akizungumza katika mkutano wa kujitambulisha kwa wanahabari msanii Tecnomile alisema Tanzania kwake ni kama nyumbani na Diamond na Vanesa  ni washikaji zake hivyo atatoa burudani kali ili washikaji wakumbuke ujio wake.



Kwa upande wake msanii Yemi ameshukuru mapokezi makubwa yaliyofanywa dhidi yao na kuwa anaipenda Tanzania na anajisikia 

yupo nyumbani na pia anakipenda Kiswahili.


Yemi alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi hasa wapenzi wa muziki kufika kwa wingi katika viwanja hivyo kupata burudani la kukata na shoka.



Wasanii wa hapa nyumbani ambao ni washindi Super Nyota 16  watakaopanda jukwaani kumsaka bingwa wa Tamasha la 

Fiesta 2016 ni  Nchama Anton a.k.aNchama, Raphael  Charles 
Manengoa.k.a Manengo kutoka (Mwanza), Ibrahim Jumaa.k.a Mpanduji(Shinyanga) , Obed  Moses   a.k.a    O strings (Muleba),
Salum Asmana.k.a Alinacha ( Kahama), Gasper Festoa.k.a   YOW (Tabora)  Alex Joseph    .a.k.a  TIZO ( Singida), Godfrey Andrew Mhojaa.k.a  NEXUS( Dodoma) Hamad Hussein  a.k.a  Med Botion (Morogoro)  Cyril Henry Isidora.k.a So Real(Tanga) Wilson Pascal     a.k.a  Willy Desmiller( Mtwara )   Charles Marikia.k.aGerere(Moshi) MohammedyAmirya.k.aCroozy (Arusha), AminaChibabaa.k.a Ammy Chiba  (Mbeya) 
Leonard John  Haulea.k.asauti classic (Sumbawanga).


Tamasha la Tigo Fiesta 2016  limekuwa  likiendeshwa kwa ubia baina Kampuni ya Prime Time Promotions na Tigo Tanzania 

huku Tigo ikiwa ndio mdhamini mkuu.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)



No comments: