ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, December 31, 2016

CROSS OVER BANQUET WITH PROPHET RICHARD STARTING SOON

HAKUNA KIINGILIO
WOTE MNAKARIBISWHA


 ADDRESS 
17009 federal hill ct bowie md

NGOMA AFRICA BAND YAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2017

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU Ughaibuni yenye makao yake nchini ujerumani inawatakia wadau wote popote mlipo heri ya mwaka mpya 2017 ,inawaombea amani,upendo na mshikamano 
Happy New Year 2017

ASKOFU MOKIWA AWAONGOZA WAUMINI WAKE KUTOA MSAADA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR ES SALAAM

 Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk.Valentino Mokiwa (katikati), akiwaongoza waumini wa kanisa hilo Archidikonari ya Kinondoni kufanya usafi katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dar es Salaam leo asubuhi wakati kanisa hilo lilipotoa msaada wa vitanda na magodoro katika hospitali hiyo vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 12.
 Waumini wa kanisa hilo wakiendelea na kufanya usafi.

HOSPITALI YA MISHENI SIKONGE YAKABILIWA NA TATIZO LA KUNGUNI

Image result for SIKONGE
Na Mussa Mbeho Sikonge

HOSPITALI ya Misheni wilayani Sikonge Mkoani Tabora inayomilikiwa na kanisa la Moravian Tanzania inakabiliwa na tatizo sugu la uwepo wa wadudu wengi aina ya kunguni hali inayohatarisha afya za wagonjwa wilayani humo.

Hayo yamebainishwa jana na Mganga Mkuu Msaidizi wa hospitali hiyo Dk John Buswelu alipokuwa akitoa taarifa ya hospitali kwa Mkuu wa wilaya hiyo Peresi Magiri aliyeambatana na Mbunge wa jimbo hilo Joseph Kakunda, Mwenyekiti wa halmashauri Peter Nzalalila na Wataalamu wa
halmashauri hiyo.

Alisema tatizo la uwepo wa kunguni hao katika Hospitali hiyo Teule ya wilaya lilianza tangu mwaka 2013 na jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanywa na uongozi wa hospitali kwa kushirikiana na wataalamu wa wadudu bila mafanikio yoyote.

MBUNGE RICHARD MBONGO AIOMBA SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WABAKAJI KATUMBA

Na Mussa Mbeho ,Katavi

WAKAZI wa kijiji cha Mtambo na Ivungwe wilayani nsimbo mkoani katavi wameilalamikia serikali ya mkoa huo kutokana na kitendo cha kushindwa kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wa jamii ya wafugaji ambao wamekuwa wakibaka wasichana na wanawake katika vijiji hivyo pindi wanawapowakuta wakichunga mifugo katika mashamba yao.

Wakazi hao wametoa malalamiko hayo leo mbele ya Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mh.Richard Philipo Mbogo katika ziara yake ya kutembelea na kusikiliza kero za wananchi wa jimbo hilo.

Wakazi hao wamesema kuwa wake zao na wasichana wadogo wamekuwa wakibakwa na kutishiwa kuuwawa kwa kutumia silaha za jadi wanazotembea nazo wakati wakichunga mifugo yao hali ambayo inadharirisha utu wa wanawake wa vijiji hivyo.

Wakazi hao ambao walikuwa wakizungumza kwa uchungu mkubwa wamesema kuwa wameshalalamika katika ngazi zote za uongozi wa mkoa huo bila kupata majibu na kuongeza kuwa endapo suala hilo halitapatiwa ufumbuzi itapelekea kuwepo kwa uvunjifu wa amani katika vijiji hivyo.

“Mheshimiwa mbunge sisi kama wananchi wa vijiji hivi kwa pamoja tunasema tumechoka kuonelewa na kubakwa kwa wake zetu na mabinti zetu na watu hawa wa jamii ya wafugaji walioingia katika maeneo haya ya kwetu bila kibali ,hivyo tunakuomba wewe mbunge wetu iombe serikali ije itatuae hili tatizo kwa watu hawa wamekuwa wakifanya vitendo hivyo bila hata kuchukuliwa hatua yeyote sasa tumechoka .Alisema mmoja wa wakazi hao .

BONDIA OMARI KIMWERI AWAMWAGIA VIFAA MABONDIA WATANZANIA

Mwakilishi wa Kimweri Promotion Nchini Tanzania Yuyuph Mnyeto kushoto akimkabidhi vifaa vya ndondi kwa kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kupokelewa na kukabidhiwa kwa wadau mbalimbali nchini vifaa hivyo vimetolewa na Bondia Mtanzania anaefanya shughuli zake Victoria, Australia, Omari Kimweri 
Bondia Selemani Kidunda kushoto kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' na Mwakilishi wa Kimweri Promotion Nchini Tanzania Yuyuph Mnyeto kushoto wakiwa katika picha wa pamoja baada ya kukabidhi vifaa vilivyotoka kwa bondia Omari Kimweri anaefanya shughuli zake Australia

BWANA WASIA MAYA NA BI. LAILA WAMEREMETA HOUSTON , TX

Siku ya Alhamis tarehe 29/12 Bw. Wasia Maya kutoka mjini Houston , Texas aliamua kuachana na kambi ya makapera na kufunga ndoa na Bi. Laila Martin. Harusi hiyo ilifanyika nyumbani kwa Bw. Wasia na kuhudhuriwa na Watanzania wengi waishio katika jiji la Houston na miji ya jirani. Ijumaa ya tarehe 30/12 kulifanyika Nikka Dinner katika ukumbi wa Pakwan uliopo kwenye makutano ya barabara za HW6 na Beechnut . Pata picha za Harusi na Nikka Dinner hapa chini

Bw. Wasia na Bi. Laila siku ya ndoa yao
Maharusi wakiwa na sura za furaha 



Bw. Wasia na mkewe Bi. Laila
Bibi Harusi Bi. Laila



Bw. Wasia

Bi. Laila

UONGOZI WA SERIKALI YA MTAA WA MARUZUKU BUGURUNI JIJINI DAR ES SALAAM WATOA SARE ZA SHULE KWA WATOTO 200

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maruzuku katika Kata ya Mnyamani Buguruni Manispaa ya Ilala, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Jabiri Sanze (kulia), akimkabidhi sare za shule mtoto, Hamad Ali Dar es Salaamleo, ambaye ataanza darasa la kwanza mwezi huu. Serikali ya mtaa huo imetoa sare za shule, daftari na penseli kwa  watoto 200 watakaoanza darasa la kwanza mwaka huu wa 2017. Katikati ni mama wa mtoto huyo, Farida Rashid.
Mtoto Issa Athumani akipokea msaada huo. Katikati mama yake Halima Issa.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AENDELEA KUFANYA MAZOEZI KWA AJILI YA KULINDA AFYA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifanya mazoezi ya viungo kwenye viwanja vya makazi yake jijini Dar es salaam ikiwa sehemu ya kuendeleza kampeni yaKitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza  aliyoizindua tarehe 17 Desemba, 2016 katika viwanja vya Leaders Club.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi na Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Oyster bay Ndugu Zefrin Lubuva ikiwa sehemu ya kuendeleza kampeni yaKitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza  aliyoizindua tarehe 17 Desemba, 2016 katika viwanja vya Leaders Club.

JUMUIYA YA WATANZANIA DMV- UFAFANUZI


Uongozi wa jumuiya ya watanzania
Unapenda kufafanua kuwa hausiki kwa njia moja au nyingine katika Party ya Mwaka Mpya inayoandaliwa hapa DMV.

Jumuiya haitahusika na athari, liability au obligations zozote zitakazo  sababishwa  na Party hiyo.

Tunategemea kufanya mchakato  wa uchaguzi  mwezi wa January 2017.

Asanteni.

Uongozi.

NI MAJALIWA ACHANGISHA FEDHA ZA UJENZI WA SHULE

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea cheti maalum cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa katika mkutano wa hadahara aliouhutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Cheti Maalum  cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa alichokabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Ali Topa   (kulia) katika mkutano wa hadhara aliouutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa wilaya ya Ruangwam Issa Njinjo.

KISOMO CHA HITMA JUMAMOSI HII.

Ndugu zetu Saidi na Nuru Mwamende wanatuarifu Kisomo cha Hitma ya Mama yao mzazi.

Tunaomba  tuudhurie  na tuwajulishe wengine.

This Saturday December 31, 2016

Argyle Local Park
1030 Forest Glen Road
Silver Spring, MD 20901

Saa TISA kamili Mchana 3pm.

Unaweza kuwasiliana na:

Saidi Mwamende 301-996-4029
Nuru Mwamende
240-603-9364
Asha Hariz
703 6242409
Iddi Sandaly
301-613-5165
Da Jasmine Rubama
410-371-9966
Asha Nyanganyi 3017932834
Ally Mikidadi 2016282133

Ahsanteni sana.

MKESHA WA MWAKA MPYA DMV

Prof Majimarefu kwenda India kwa matibabu

VAZI LA KHANGA KUTUFUNGIA MWAKA 2016 PALE REGENCY PARK HOTEL DON’T MISS!

Ni jambo la kufurahisha kutoka kwenye Tasnia Mitindo hapa Tanzania kutokana na jinsi ambavyo wadau hao wa mitindo wamejipnga kufanya maajabu ya ki-Fashion katika tukio kubwa la kuuaga mwaka 2016 na Vazi la Khanga, kupitia ile event matata maarufu kama “Khanga Party “ Party ya kijanja ambayo huandaliwa kila mwaka na Mama wa Mitindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin.

Katika Party hiyo kutakuwa na Designers wa kutosha plus wadau mbalimbali wa mitindo bila kusahau Surprise kibao za Burudani ziki pambwa na mitoko ya Khanga. Kumbuka Party hii itafanyikia pale Regency Park Hotel siku ya Jumamosi 31/December /2016 kuanzia mida ya saa mbili kamili usiku.

Tafadhali tunaomba support yako katika tukio hili muhimu na lakipekee ili tuweze kuuanga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya 2017 kwa furaha za Shangwe, upendo na mshikamano kutoka kwa wanamitindo wote wa hapa Tanzania. Asante.

MKUU WA WILAYA YA ROMBO,AGNES HOKORORO AKAMATA NA KUTEKETEZA LITA 4000 YA POMBE CHAFU.

Mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo akiangalia namna pombe ya kienyeji inavyoandaliwa baada ya kukamata kiwanda bubu cha kutengenezea pombe bila ya kufuata taratibu.
Mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe ya kienyeji  aliyefahamik kwa jina moja la Carlos akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo namna wanavyoandaa pombe hiyo.

KAIMU KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AWAASA MAOFISA MAGEREZA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA UFANISI

Na Lucas Mboje, Dar es Saam
KAIMU Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa(pichani) amewaasa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza  nchini kuzingatia  kuwa utendaji wao wa kazi za kila siku uende sambamba na kasi ya Serikali ya Awamu ya tano ili kuleta ufanisi unaotarajiwa.

KAIMU Kamishna Jenerali, Dkt. Malewa ameyasema hayo jana wakati wa Baraza la Kufunga Mwaka 2016 na kuukaribisha Mwaka 2017 lililowahusisha baadhi ya Maafisa na Askari kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani pamoja na Magereza ya Mkoa wa D'Salaam.


Aidha, amewataka Maofisa na Askari wa Jeshi hilo kudumisha nidhamu wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kazi  ikiwemo kutekeleza mara moja Amri mbalimbali zinazotolewa na Viongozi wao wa Jeshi.

KAIMU KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AHUTUBIA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA 2016 NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2017 JIJINI DAR


Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba yake fupi ya kufunga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya 2017 kwenye Baraza la Maafisa na Askari kutoka vituo mbalimbali vya Magereza Mkoani Dar es Salam Desemba 30, 2016 katika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga.

Naibu Kamishna wa Magereza, Edith Mallya akimkaribisha Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati aliyeketi) kabla ya kuongea na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya 2017(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa D ar es Salaam, SACP. Augustine Mboje. Baraza hilo limefanyika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam Desemba 30, 2016.

Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akijibu kero mbalimbali zilizoulizwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam(hawapo pichani) katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya 2017

MAONI YA WATEJA NI MUHIMU KWA UKUAJI WA BIASHARA YAKO

Na Jumia Travel Tanzania

KUJA kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia hususani mtandao wa intaneti kumebadilisha kwa kiasi kikubwa mienendo ya matangazo ya utoaji wa huduma mbalimbali duniani na hii ni kutokana na uwezo wake wa kuwaruhusu wateja kutoa ushuhuda, kukosoa au kutoa maoni juu ya walichohudumiwa na kujionea.

Tofauti na kipindi cha nyuma kidogo ambapo wataalamu wa masoko walikuwa wanatumia zaidi njia za luninga na redio kuwafikia wateja wao, siku hizi mfumo wa intaneti unapewa kipaumbele zaidi kutokana na namna unavyofikia watu wengi zaidi ndani ya muda mfupi, kwa haraka na gharama kidogo.

Matangazo ya luninga na redio yanaweza kuwa hayana ushawishi mkubwa ukilinganisha na mtandao wa intaneti kwani hivi sasa makampuni yanaweza kuwasilisha bidhaa na huduma zao na kupokea majibu kujua kwamba zinakubalika au la. Hali hiyo ni dhahiri kutokana na makampuni mengi kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika teknolojia na rasilimali watu katika kusimamia tovuti na kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter, instagram na mingineyo.

Kupitia tovuti na kurasa hizo za mitandao ya kijamii biashara na huduma nyingi zinafanya vizuri kutokana na ushawishi wao kwenye mitandao kutokana na namna ambavyo zinazungumziwa vizuri na watu wengi. Lakini pia husaidia kampuni hizo husika kuwasiliana moja kwa moja na wateja wao kwa sababu wateja huwasilisha maoni yao moja kwa moja mtandaoni tofauti na luninga au redio ambazo hutoa fursa ya kuona au kusikiliza tu matangazo.

Vivyo hivyo hali hii inaweza kusaidia sana ukuaji wa sekta ya utalii na ukarimu kama vile huduma za hoteli na malazi ambazo hujitangaza zaidi kupitia namna wateja wanavyozizungumzia.

Jumia Travel (www.travel.jumia.com) kampuni unaongoza kwa huduma za hoteli mtandaoni barani Afrika umezitunuku vyeti hoteli kadhaa ambazo zilizopendekezwa na kutembelewa ndani ya wateja wengi kipindi cha mwaka mzima wa 2016.

Akizungumzia juu ya umuhimu wa vyeti hivyo Meneja Mkazi wa Jumia Travel Tanzania, Bi. Fatema Dharsee amesema kuwa, “Vyeti hivi vina umuhimu mkubwa kwani ni viashiria vikubwa vya namna hoteli yako inatathminiwa vipi na wateja pindi wanapoitembelea. Siku zote wateja huambizana huduma wanazozipata sehemu za biashara wanazotembelea na kutokana na ushuhuda huo ndio na wengine hushawishika kutembelea pia. Kupitia mtandao wetu wateja wanayofursa ya kutoa maoni juu ya hoteli walizozitembelea, huduma walizopatiwa, mapungufu waliyoyaona na maboresho ambayo wangependa yafanyiwe kazi.”

MBUNGE MUSSA WA JIMBO TANGA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA WAKULIMA JIMBONI MWAKE

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku kulia akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kikundi cha Golani Shutashuta,Saidi Bakari  wakati alipokwenda akikagua mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji eneo la Golani Shutashuta Kata ya Pande Jijini Tanga jana wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea kuona namna wanavyotekeleza majukumu yao na changamoto ambazo zinawakabili
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikangalia naamna mradi huo unavyopandwa

OFISI YA KIJIJI CHA MTYANGIMBOLE YA CHOMWA MOTO - RUVUMA

 Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti   Mgema akionyesha moja ya sehemu ambayo moto bado unawaka .
 Hiyo ndiyo hali halisi ya ofisi jinsi ilivyoungua kwa ndani

MSAJILI MKUU WA MAHAKAMA AWATAKA MAHAKIMU WAZINGATIE HAKI YA DHAMANA

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Katrina Revocati amewataka mahakimu nchini kuzingatia sheria katika utendaji wao wa kazi hasa katika utoaji wa dhamana. 

Kauli ya Msajili imekuja wakati kukiwa na malalamiko dhidi ya baadhi ya mahakimu kuwanyima dhamana washtakiwa ilhali mashtaka yao yanaruhusu. 

Aidha, kauli ya msajili huyo mkuu imekuja wakati mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakipambana ili mteja wao apate dhamana baada ya kukwaa kisiki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha. 

Mashtaka ambayo kwa mujibu wa sheria dhamana zake zimezuiwa ni ya mauaji ya kukusudia, uhaini, utakatishaji wa fedha, wizi wa kutumia silaha, usafirishaji binadamu na dawa za kulevya. 

MAGAZETI YA LEO DESEMBA 31, 2016

Friday, December 30, 2016

Funeral Fund

Inna Lillah Wa Inna Ilayhi Rajiun.
Our beloved father, uncle, brother, and friend to many, Mr. Ubwa Jaha has passed away on Dec 29, 2016. his Funeral and burial services will be held on Sat. Dec 31, 2016 at 12:30 pm in Bellevue Washington, USA.

Kindly, we ask for your generous donation to cover the funeral and burial cost that are being estimated to be 4,000 dollars.

We will greatly appreciate for anything that you may be able to donate for the purpose of laying our beloved one to rest.

Please Tap HERE to donate

Thank you all.
Help spread the word!

LOOK OF THE DAY

JAQ AMANI WA DAR-ES-SALAAM

BONDIA FRANCIS CHEKA AFUNGIWA KWA MIAKA MIWILI

KAMISHENI ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) imemfungia Bondia Francis Cheka kushiriki katika mchezo wa ngumi kwa kipindi cha miaka miwili na kulipa faini ya shilingi laki tano kwa kitendo cha kukacha pambano baina yake na Bondia Abdallah Pazi (Dulla Mbabe).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Msaidizi wa TPBC, Chatta Michael alisema kamisheni hiyo ilitoa kibali cha pambano kati ya Cheka na Abdallah Pazi lakini bondia huyo hakufika katika pambano hilo huku akiwa ameshalipwa kiasi cha shilingi milioni tatu.

Chatta alisema kuwa Cheka aliaharisha pambano hilo lililokuwa lifanyike katika ukumbi wa Sabasaba tarehe 25 Desemba mwaka huu pasipo na kutoa taarifa, wakati Promota wa pambano hilo alikwishaingia gharama mbalimbali za maandilizi ya pambano hilo.

“Kamisheni imejiridhisha kuwa kiasi cha shilingi milioni tatu kilitolewa  kwa Francis Cheka kabla ya pambano, hivyo alitakiwa apatiwe kiasi kilichobaki baada ya pambano kama alivyokubali na kusaini mkataba wa pambano hilo,” alifafanua Chatta.

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MJINI RUANGWA

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Ruangwa wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya  hiyo kuhutubia mkutano wa hadhara Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya  Ruangwa Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ZITTO KABWE ATOA TAMKO KUHUSU RASILIMALI NA MADENI YA TAIFA

Ndugu Watanzania, Kama mnavyofahamu kuwa ibara ya 132(4) na (5) na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria namba 13 ya mwaka 1995 inataka viongozi wote wa umma kujaza fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni. Tamko hilo huwasilishwa Sekretariat ya Maadili ya Viongozi kabla ya mwisho wa kila mwaka. Kama nifanyavyo siku zote, nawajulisha rasmi kwamba nimetimiza matakwa hayo ya katiba na sheria kuhusu Maadili ya Viongozi.

Inafahamika kuwa Chama Cha ACT Wazalendo, kwa mujibu wa Katiba yake na Azimio la Tabora, kimeelekeza kuwa Viongozi wake wote waweke wazi kwa Umma Tamko la Mali, Madeni na Maslahi. Kwa kufuata masharti ya Katiba ya Chama Cha ACT Wazalendo natangaza rasmi fomu zangu nilizowasilisha Leo Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Ni matumaini yangu kwamba itafikia wakati Daftari la Rasilimali na Madeni la Viongozi wa Umma litakuwa linawekwa wazi kwa Umma ili wananchi waweze kujua Mali, Madeni na Maslahi ya Viongozi wao na pale ambapo kiongozi ametoa habari zisizo sahihi au kuficha mwananchi aweze kutoa Taarifa kwenye Sekretariat na Baraza la Maadili liweze kufanya kazi yake ipsavyo.

NEW YEAR'S EVE PARTY DURHAM, NC

KICHUPA CHA LEO RICH MAVOKO FT DIAMOND PLATNUMZ - KOKORO ( OFFICIAL VIDEO)

MWAMOYO HAMZA NDANI YA VOA STUDIO 15 MOMBASA NCHINI KENYA

Mkuu wa VOA Swahili Dr. Mwamoyo Hamza akipata ukodak moment mapema leo Ijumaa Desemba 30, 2016 ndani ya VOA studio 15 Mombasa iliyozinduliwa hivi karibuni
Dr. Mwamoyo Hamza mkuu wa VOA Swahili akijipendelea na ukodak ndani ya VOA studio 15 Mombasa nchini Kenya mapema leo Ijumaa Desemba 30, 2016.

UPDATE YA MSIBA WA UBWA JAHA

Ubwa Jaha enzi ya uhai wake
Tunatarajia kufanya mazishi ya ndugu yetu, marehemu Ubwa Jaha, siku ya Jumamosi:Desemba 31, 2016, baada ya sala ya adhuhuri 12:30pm. Maiti itasaliwa msikiti wa Bellevue, Washington.

Kwa taarifa hii tunaomba mchango wa haraka wa fedha kwa ajili kufanikisha mazishi hayo.
Gharama inayotukabili ni dola elfu nne ($4,000).

Hivi sasa maiti imehifadhiwa funeral home, Kent. Kadiri tutakavyochelewa, gharama zinapanda zaidi.

Tafadhali pitisha mchango wako:
Bank of America.
Ahmed Kayanda.
Acct. 68316520

Au wasiliana na mimi (425) 890-7428.

Tafadhalini sana tushirikiane katika hili.

Ahsante.
Ahmed

EWURA YARIDHIA KWA SEHEMU OMBI LA TANESCO KUPANDISHA BEI YA UMEME

MAMLAKA ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA), imetangaza ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 8.5%.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlamgosi, (pichani), ongezeko hilo la bei ni kufuatia maombi ya Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), ambalo liliwasilisha maombi EWURA ya kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari mwaka 2017.

Akitangaza bei hizo mpya jijini Dar es Salaam, leo Mkurugenzi Mkuu huyo wa EWURA amesema, baada ya kufanya uchambuzi wa kina, Mamlaka yake imefikia uamuzi wa kuongeza asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017 kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wake.

Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa kwa asilimia 5.7% ya bei ya umeme.

Hata hivyo ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao hayazidi uniti 75 kwa mwezi.

Kundi la TIB linalohusisha viwanda vidogo, mabango na minara ya mawasiliano litakua na tozo ya mwezi ya shilingi 5,520.

Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), linaendelea kufanya maboresho ya miundombinu ya umeme na kutekeleza miradi mipya ya kuunganisha wateja ili kuboresha huduma za umeme nchini.