ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, December 31, 2016

MBUNGE RICHARD MBONGO AIOMBA SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WABAKAJI KATUMBA

Na Mussa Mbeho ,Katavi

WAKAZI wa kijiji cha Mtambo na Ivungwe wilayani nsimbo mkoani katavi wameilalamikia serikali ya mkoa huo kutokana na kitendo cha kushindwa kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wa jamii ya wafugaji ambao wamekuwa wakibaka wasichana na wanawake katika vijiji hivyo pindi wanawapowakuta wakichunga mifugo katika mashamba yao.

Wakazi hao wametoa malalamiko hayo leo mbele ya Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mh.Richard Philipo Mbogo katika ziara yake ya kutembelea na kusikiliza kero za wananchi wa jimbo hilo.

Wakazi hao wamesema kuwa wake zao na wasichana wadogo wamekuwa wakibakwa na kutishiwa kuuwawa kwa kutumia silaha za jadi wanazotembea nazo wakati wakichunga mifugo yao hali ambayo inadharirisha utu wa wanawake wa vijiji hivyo.

Wakazi hao ambao walikuwa wakizungumza kwa uchungu mkubwa wamesema kuwa wameshalalamika katika ngazi zote za uongozi wa mkoa huo bila kupata majibu na kuongeza kuwa endapo suala hilo halitapatiwa ufumbuzi itapelekea kuwepo kwa uvunjifu wa amani katika vijiji hivyo.

“Mheshimiwa mbunge sisi kama wananchi wa vijiji hivi kwa pamoja tunasema tumechoka kuonelewa na kubakwa kwa wake zetu na mabinti zetu na watu hawa wa jamii ya wafugaji walioingia katika maeneo haya ya kwetu bila kibali ,hivyo tunakuomba wewe mbunge wetu iombe serikali ije itatuae hili tatizo kwa watu hawa wamekuwa wakifanya vitendo hivyo bila hata kuchukuliwa hatua yeyote sasa tumechoka .Alisema mmoja wa wakazi hao .

Nao viongozi wa kata ya katumba Mh.Seneta Baraka na Kaimu afisa mtendaji wa kata hiyo Bw.Felix Kuhoma wamekiri kupokea malalamiko ya wakulima wa vijiji hivyo vya kutishiwa,kupigwa ,kuuwawa pamoja na kubakwa kwa wanawake pindi wafugaji hao wanapozuiliwa na wakulima kurisha mifugo katika mazao yao huku wakisema kuwa wafugaji hao hawakuruhusiwa kuingiza mifugo katika vijijiji hivyo.

Kwa upande wake,Mbunge wa jimbo la Nsimbo Mh.Richard Philipo Mbogo,ameuagiza uongozi wa Halmshauri ya Wilaya kumwandikia haraka barua mkuu wa Wilaya hiyo ili aweze kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo kabla hayatokea matatizo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kufanya vitendo vya ubakaji kwa wanawake wa vijiji hivyo.

Katika hatua nyingine Mh.Mbogo amekemea viashiria vya kibaguzi katika matumizi ya ardhi vinavyofanywa na baadhi ya wakazi wa jimbo hilo vinatakiwa kumalizwa haraka kwani watanzania sote ni ndugu na hakauna mwenye aridhi yake hapa duniani.

Hata hivyo Mh Mbogo ameongeza kuwa Migogoro ya wakulima na wafugaji inayohusha matumizi ya ardhi na kuepelekea mauaji imekuwa ikitajwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo Morogoro,Mara na Arusha hivyo serikali ichukue hatua za haraka kumaliza tatizo hilo katika vijiji hivyo.

mwisho

No comments: