Kampuni ya ndege ya Bombardier inatarajia kuzileta ndege tatu mpya kwaajili ya shirika la ndege la Tanzania, ATCL, imefahamika.
Mwishoni mwa Septemba mwaka huu, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli aliahidi kununuliwa kwa ndege zingine mbili kubwa kwaajili ya shirika la ndege la Tanzania, ATCL.
Alitoa ahadi hiyo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa ndege mbili mpya za kwanza kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Ndege hizo ni aina ya Bombadier Q 400 zilizotengenezwa nchini Canada.
Alisema ndege mbili kubwa zitakazonunulia hapo baadaye zitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 160 na nyingine kubwa zaidi itakayobeba abiria 240 pamoja na mizigo yao. Aliwahakikishia Watanzania kuwa fedha za kununua ndege hizo zipo.
Ndege za sasa zina uwezo wa kubeba abiria abiria 76, 6 wakiwa daraja la juu na 70 ni daraja la chini
Credit::Bongo5.com
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake