Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemnyima dhamana Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema. Mahakama hiyo imeeleza kuwa mawakili wamtuhumiwa huyo walipaswa kuonesha kusudio la kukata rufaa ndani ya siku10 kabla ya kukata rufaa.
Hii ni mara ya tano mbunge huyo anakosa dhamana mahakamani tangu alipokamatwa Novemba 3 mwaka huu akiwa mjini Dodoma na kusafirishwa hadi Arusha katika kesi ya uchochezi inayomkabili.
Katika kesi ya msingi lema anatuhumiwa kutoa maneno ya kichochezi dhidi ya Rais Magufuli kwa madai kuwa Mungu ndiye aliyemwambia maneno hayo wakati akiwa anaomba.
Nini kilichoko nyuma ya pazia kuhusiana na hilinswala la Lema Mbunge!? Kama ni adhabu si itolewe mbona kuna kesi za kufanya hili la Lema ni amri toka Juu. Milioni 10 mbona hazifanyiwi kazi?
ReplyDelete