Friday, December 2, 2016

RC ARUHUSU MJANE KUJENGA ENEO AMBALO POLISI WAMEZUIA KUJENGA

Mkuu wa mkoa wa njombe Dr Rehema Nchimbi Akizungumza na wafanyakazi wa halmashauri ya Makambako (Picha Hapo Juu)
Badhi ya watumishi wa halmashauri ya Mji Makambako wakimsikiliza mkuu wa mkoa alipo fika katika Halmashauri yao kujia shina ma matatizo yao (Picha Hapo Chini)

SERIKALI mkoani Njombe imetoa ruhusa ya kujenga nyumba mama mjane ambaye amezuiriwa na Jeshi la polisi wilaya ya kipolisi Makambako kutokana na eneo hilo kuwa na mgogoro baina yake na jeshi hilo kwa kuwa majirani wa mama huyo wameruhusiwa kujenga.

Kauli hiyo inatolewa na mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi baada ya kupata taarifa za kuwapo kwa mkanganjiko wa kiwanja cha mjane huyo na kuwapo kwa mvutano mrefu baina ya yake na jeshi la polisi wakati akiwa na mkotano na watumishi wa halmashauri ya mji Makambako ambako yupo katika ziara ya kikazi mkoani humo.

Dr. Nchimbe anasema kuwa mama huyo ajenge kama majirani zake walivyo ruhusiwa kujenga maeneo hayo na wakati watakavyo bomoa kwa majirani wengine basi wabomoe kwa wao wote.

Alisema kuwa haiwezekani mama huyo akazuiliwa kujenga wakati wajirani zake wameruhusiwa kujenga na kuwa kwa kuwa watu hao walijenga kiholele basi hata mama huyo ajenge kiholela.

Hata hivyo mkuu wa mkoa aliingia katika majibizano ya maswali na majibu na afisa mipango walipo kuwa akimuhoji afisa mipango wa halmashauri hiyo Ephahim Mkambo.

Mkuu wa mkoa: kwanini mama huyo haruhusiwi kujenga.

Afisa mipango: mama huyo yupo katika eneo la polisi na haruhusiwi kujenga eneo hilo.

Mkuu wa mkoa: Kwanini majirani zake waliruhusiwa kujenga, eneo hilo.

Afisa mipango: Hawa wengine walijenga kiholela na wenye eneo walishindwa kudhibiti mikapa yao.

Mkuu wa Mkoa: sasa naamuru naye huyu mama ajenge eneo hilo kihilele na watakapo kuwa wakibomoa wabomolewe wote haiwezekani akazuiwa mmoja na wengine wakaruhusiwa.

Mkuu wa mkoa baada ya kutoa ruhusa ya ujenzi kwa mjane huyo alimuonya mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Makambako Paulo Malala kuto saini karatasi za watu wa ardhi kwa kuwa wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao kwa usahihi na kufanya kwa ujanja ujanja.

“Nakuonya Mkurugenzi wewe usisaini karatasi za watu wa ardhi watakuingiza matatani hawa ni wajanja wajanja kuwa majini nao,” alisema Dr. Nchimbi.

Katika mkutano wake huo na maafisa na wakuu wa Idara walitoa maoni yao mbalimbali na changamoto zao ambazo zinawakabili kutekeleza majukumu yao na kufanya kazi za wananchi.

Afisa utumishi wa halmashauri hiyo Frederick Kazikuboma alisema kuwa halmashauri hiyo inaupungufu wa magari, na rasisimali watu ambapo kuna idara zinawafanyakazi wacheche.

Hata hivyo Dr. Kyunga Ernest, ni Afisa afya na ustawi wa jamii Halmashauri ya Makambako alisema kuwa pamoja na kuwa na kituo cha afya katika halmashauri hiyo changamoto kubw ani kuto kuwapo kwa chumba cha upasuaji licha ya kuanza ujenzi wake na baadhi ya vifaa kuwanavyo.

Alisema kuwa pamoja na changamoto hiyo halmashuri imekuwa ikipokea fedha za kituo cha afya huku huduma zinazotolewa zikiwa ni za hospitali kutokana na watu wanaofika Hospitalini hapo.

Alisema kuwa baada ya kufunga mfumo wa kielekroniki wa kukusanya mapato wamekuwa wakikusanya zaidi ya milioni 14 lakini watu wanaopata huduma za bure hupokea watu wanao hudumiwa kwa gharama ya Milioni 13 au zaidi ya milioni 14 kitu ambacho hushindwa kujiendesha kwa fedha za ndani.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake