Wednesday, December 7, 2016

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAPOKEA MSAADA WA JEZI NA MIPIRA KUTOKA KAMPUNI YA SANLAM LIFE INSURANCE.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Hamidu Athuman (kushoto) akipokea msaada wa jezi kutoka kwa Kamimu Mkurugenzi Mtendaji wa Sanlam Life Insurance Ndg. Mika Samwel (kulia) mapema leo asubuhi katika Makao Makuu ya ofisi hizo zilizopo mtaa wa Ohio.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Hamidu Athuman (kushoto) akipokea msaada wa jezi kutoka kwa Kamimu Mkurugenzi Mtendaji wa Sanlam Life Insurance Ndg. Mika Samwel (kulia) mapema leo asubuhi katika Makao Makuu ya ofisi hizo zilizopo mtaa wa Ohio.
Meneja Mahusiano wa Sanlam Life Insurance Ndg. Rishia Kileo wa kwanza kushoto akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji kwa ugeni toka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji uliotembelea makao makuu ya ofisi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Sanlam Life Insurance Ndg. Mika Samwel wa tatu kutoka kulia akiwa kwenye pichani ya pamoja na Viongozi waliomuwakilisha Kamishna Jenerali kupokea msaada huo. (Picha na Godfrey Peter – Jeshi la Zimamoto)

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Hamidu Athuman amepokea msaada wa jezi na mipira kwa niaba ya Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi kutoka kwa Kampuni ya SANLAM LIFE INSURANCE katika msaada huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Mika Samwel alikabidhi Jezi jozi mbili na mipira kumi zenye thamani ya fedha za kitanzania shilingi milioni mbili na laki tano.

Akikabidhi msaada huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo amewaasa viongozi na wachezaji wa timu hiyo kutumia vema msaada huu katika mashindano hayo yatakayoshirikisha timu za majeshi (BAMATA) katika michezo itakayofanyikia Visiwani Zanzibar hivi karibuni.Naye Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo alimshukuru kwa niaba ya Kamishna Jenerali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na uongozi wa Kampuni hiyo kwa msaada walioutoa. Aidha alimuahidi kuutumia vema msaada walioupata na kumuhakikishia ushindi katika michezo hiyo pia aliwahasa wadau wengine kujitokeza kuisaidia timu hiyo.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake