Advertisements

Thursday, December 1, 2016

MAKAMBA AONGEA NA WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba akiongea na Wahahariri wa Jukwaa la Wahariri (hawapo pichani) kuhusu ziara ya mazingira aliyoifanya katika mikoa mikumi Nchini Tanzania manamo mwezi wa Novemba. Aliyeko katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbarak Abdulwakil na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Richard Muyungi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba akionyesha kwa Wahariri wa vyombo vya habari, picha tofauti za maeneo mbalimbali aliyotembelea wakati wa ziara yake ya kutembelea Mikoa 10 Nchini kuangalia athari za mazingira.
Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Richard Muyungi akiongea wakati wa Mkutano huo.
Sehemu ya Wahariri na Waaandishi wa Habari mbalimbali waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba alipoongea nao Ofisini kwakae kuongelea ziara yake aliyoifanya kwa mikoa 10 Nchini
Mhariri wa gazeti la Jamhuri Jackton Manyerere akichangia mada wakati wa Mkutano huo na Waziri Makamba .

No comments: