Saturday, December 10, 2016

Meli yawasili Mtwara na malori 651 ya Dangote

 Muda mfupi baada ya Alhaj Aliko Dangote kumaliza kikao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli,  na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu uzalishaji wa kiwanda chake, kiwanda cha utengenezaji saruji cha Dangote kimeshuhudia kuwasili kwa meli ya Morning Composer Panama ikiwa na malori 651 tayari kwa kusaidia uzalishaji wa kiwanda hicho.
Kwa mujibu wa wenzetu wa Pride Fm iliyo Mtwara, meli hiyo kubwa iliyo na urefu wa zaidi ya viwanja viwili vya mpira wa miguu (soka) iliwasili jioni ya leo kwa majira ya Tanzania na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dr Khatib Kazungu.
Meli hiyo iliingizwa gatini na Nahodha Mkuu wa bandari zote za kusini Hussein Kasuguru, ambaye baada ya kuegesha, alizungumza na waandishi wa habari. Msikilize

Baada ya hapo, James Lemomo, Meneja uendeshaji wa kampuni ya Diamond Shipping alizungumza na waandishi wa habari

Kisha, Mkuu wa wilaya Dr Kazungu, alizungumza na waandishi wa habari

 
 
 


No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake