Advertisements

Saturday, December 10, 2016

RAIS MAGUFULI AOMBA RADHI

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaomba radhi watanzania ambaowalichukizwa na maamuzi yake aliyoyafnya mwaka jana ya kufuta sherehe za uhuru na badala yake kutumia pesa kwenye upanuzi wa barabara. Rais Magufuli ameomba msamaha wakati akitoa salamu zake za maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru, katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, ambapo alitumia nafasi hiyo kueleza sababu za kufuta sherehe hizo mwaka jana na kuziruhusu mwaka huu.
Rais Magufuli amesema sababu mbili mojawapo ikiwa ni kuokoa pesa ambazo zilikuwa zimepangwa kutumiwa na watanania wachache katika sherehe zile na kuamua kuzielekeza kwenye matumizi ambayo watanzania wote watafaidika.
Amesema kama kuna watu ambao aliwaudhi kwa maamuzi hayo wamsamehe lakini kama pia kama wapo waliofurahia maamuzi hayo, anawashukuru.
"Mwaka jana nilipouliza shilingi ngapi zimetengwa kwa ajili ya sherehe nikaambiwa bilioni 4, nikauliza hizi bilioni nne kuna wageni au kuna nini, wakasema ni pamoja na chakula kwa wageni, posho na mambo mengine, nikaona bilioni nne zinataka kutumiwa na watanzania wachache, nikaamua ni bora zikajenge barabara ili watanzania wote wafaidi, kama kuna watu watu hawakupenda, wanisamehe sana" Amesema Rais Magufuli.

2 comments:

Anonymous said...

tuliambiwa hizi sherehe ni kma kuharibu fedha za walipa kodi, tuna mabo mengi muhimu yanatuhitaji, je mahitaji yamekwisha?

Anonymous said...

Uta umiza kichwa kwa maswali yasio na majibu