Wednesday, December 7, 2016

RIPOTI YA MADAKTARI KUHUSU CHANZO CHA KIFO CHA MCHEZAJI WA MBAO FC

Ripoti iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dk. Thoma Rutta na kusomwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi inaeleza kuwa kusimama kwa moyo ghafla  ndio chanzo cha kifo chipukizi wa Mbao FC ya Mwanza, Ismail Khalfan Mrisho.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na kamanda huyo alipokuwa akizungumza kuelezea chanzo cha kifo cha mchezaji huyo kilichotokea Jumapili wakati wa mchezo wa Mbao FC dhidi ya Mwadui FC ikiwa ni ligi ya vijana katika uwaja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Daktari ametoa taarifa ya uchunguzi na kusema chanzo ni kusimama kwa moyo ghafla. Marehemu hakuwa na jeraha lolote, alisema Kamanda Ollomi.


Ismail Mrisho alizaliwa Mei 22, 1997 akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia yao. Amesoma Shule ya Msingi Nyakabungo kuanzia mwaka 2006 hadi 2012. Mwana 2013 alijiunga na Sekondari ya Mwanza ambapo alihitimu mwaka 2016. Ismail alikuwa amepata ufadhili wa kwenda kusoma Chuo Kikuu cha Louisiana State nchini Marekani kuanzia mwakani.

Ismail lifikwa na mauti muda mfupi baada ya kugongana na mchezaji wa Mwadui, alipojaribu kusimama baada ya hapo alianguka tena ndipo alipokimbizwa hospitali mjini Bukoba lakini akafariki. 

Kabla ya kukumbwa na mauti hayo, aliifungia timu yake ya Mbao goli la kuongoza ambapo mchezo ulimalizika kwa Mbao kupata ushindi wa 2-0.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake