ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 7, 2016

WAAMUZI WAONDOLEWA RATIBA YA LIGI KUU YA TANZANIA BARA

Waamuzi waliochezesha mchezo namba 49 kati ya Yanga na Simba, Martin Saanya na Samweli Mpenzu wametolewa kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, huku suala lao likipelekwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili ishughulikie tatizo lao kitaalam. 


Maamuzi hayo yamefanyika baada ya Kikao cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya ligi, kuwaita na kuwahoji na kuangalia mkanda wa mchezo husika. Kamati imebaini mapungufu mengi ya kiutendaji yaliyofanywa na waamuzi hao, na hivyo kuitaka kamati ya waamuzi ishughulikie. 

Pia Mwamuzi Rajabu Mrope aliyechezesha mchezo namba 108 kati ya Mbeya City na Yanga naye ametolewa kwenye Ratiba ya Ligi Kuu  msimu 2016/2017 na kurudishwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili waweze kumpangia daraja lengine la uamuzi. 


Mrope alitiwa hatiani kwa kosa la kutojiamini mchezoni na kwenye uamuzi wake na kushindwa kuudhibiti mchezo. 

Miongoni mwa matatizo ya mwamuzi huyo ni kukubali goli, kisha kukataa na mwisho kukubali tena hali iliyoonyesha kutokujiamini na kusabisha mtafaruku mkubwa katika mchezo huo. 

Katika ligi ya Daraja la kwanza, Mwamuzi Thomas Mkombozi aliyechezesha mechi namba 15B kati ya Coastal Union na KMC ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kutokana na kushindwa kuudhibiti mchezo na kutoshirikiana na wasaidizi wake. 

Adhabu hiyo ametolewa baada ya Kamati ya usimamizi na uendeshaji wa ligi kuwaita waamuzi wa mchezo huo na kufanya mahojiano nao na kugundua Mkombozi alikuwa na maamuzi mengi bila umakini na hakushirikiana kiufundi na wasaidizi wake. Kutokua makini kulisababisha mchezo huo kumalizika kwa vurugu. 

Pia Klabu ya Coastal Union imepewa adhabu ya kucheza bila ya mashabiki kwa mechi mbili za nyumbani na mechi moja ya nyumbani kuchezwa uwanja wa ugenini kwa kosa la mashabiki wa timu hiyo kumshambulia Mwamuzi Thomas Mkombozi na kumsababishia majera ha maumivu makali. 

kuhusu Mwamuzi Ahmed Seif, Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya bodi ya Ligi, imemfungulia na kumtoa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi kuu mwamuzi huyo aliechezesha mchezo namba 28 kati ya African Lyon na Mbao FC. hivyo, Mwamuzi Ahmed Seif atarudishwa kwenye kabati ya waamuzi ili apangiwe majukumu mengine.


No comments: