
Wakazi wa kijiji cha Katumba na Kaminula katika halmashuri ya wilayani nsimbo mkoani katavi wako hatarini kukumbwa na mlipuko wa wa ugonjwa wa kipindu kufuatia Kujaa kwa vyoo katika kituo cha afya Katumba na zahanati ya Kaminula hali ambayo inapelekea wagonjwa kujisaidia ovyo vichakani pindi wanapokwenda kupatiwa huduma za afya .
Hayo yamebainishwa jana na Mganga mfawidi wa kituo cha afya cha Katumba Dkt Gabriel Ngonyani na Mganga mfawidhi wa zahanati ya Kaminula Dkt Ismail Bane katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika wiwanja vya Ofisi za kijiji cha Kambuzi A wiyani hapa.
Wamesema kutokana na kujaa kwa vyoo katika zahanati na kituo hicho cha afya kunauwezekanao mkubwa wa kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu kwani wagonjwa wengi wamekuwa wakikimbilia kujisaidia kwenye vichaka ambavyo viko karibu na makazi ya watu .
Nao baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo wamesema kuwa wameshalalamika kwa muda mrefu katika uongozi wa serikali za vijiji lakini wamekuwa hawapati majibu ya kutosha na kumuomba mbunge wa jimbo hilo Mh.Richard Philipo Mbogo kuwasaidia ili kuweza kuchimba vyoo vingine katika zahanati pamoja na kituo hicho cha afya.
Sambamba na hilo wakazi hao wamsema kuwa , pamoja na changamoto hiyo,pia kuna changamoto ya Ukosefu wa umeme ,maji safi na salama, uhaba wa watumishi, na uchakavu wa majengo katika zahanati ya kaminula na kituo cha afaya katumba hali ambayo inapelekea kuwepo kwa huduma mbovu za afya .
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mh.Richard Philipo Mbogo, ameziagiza kamati za afya za Kituo cha Katumba,Zahanti ya Kaminula kuanisha mahitaji yote kwa ujumla yanayohitajika na kuyasilisha katika ofisi yake ili hatua za utatuzi zifanyike haraka iwezekanavyo.
Aidha Mh.Mbogo amewatoa hofu wakazi wa vijiji hivyo na kusema kuwa Ujenzi visima vya maji katika jimbo hilo unatarajiwa kupewa kipaumbele katika bajeti ya shilingi milioni 480 iliyotengwa na hamashauri hiyo katika mwaka wa fedha 2017/2018.
No comments:
Post a Comment