Wednesday, December 7, 2016

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DKT. PHILIP MPANGO ATETA NA BALOZI WA JAPAN NCHINI, MASAHARU YOSHINDA

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akisisitiza jambo kuhusu kuharakisha maendeleo ya ujenzi wa miundombinu itakayokuwa chachu ya kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda, wakati Balozi wa Japan na ujumbe wake walipomtembelea na kufanya mazungumzo na Waziri huyo Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa kwanza kulia) akisikiliza maelezo toka kwa Mwakilishi Mkazi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Japani (JICA) kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa ujenzi wa barabara mkoani Arusha na maeneo mengine ya nchi, Kikao hicho kimefanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.

 Balozi wa Japani Nchini Tanzania, Masaharu Yoshinda (kushoto) akielezea mtazamo wake kuhusu umuhimu wa kufungua mikoa ya Kanda ya Kati na Magharibi mwa Tanzania kwa miundombinu ikiwemo barabara na reli ambayo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.  Dkt. Philip Mpango (Mb) alimweleza Balozi huyo kuwa ina faida kwa maendeleo ya nchi, walipokutana na kufanya mazungumzo Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
 Balozi wa Japani Nchini Tanzania Masaharu Yoshinda (kushoto) na Mwakilishi Mkazi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Japani (JICA) Bw.  Toshio Nagase, (kulia), wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani) kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo inayofadhiliwa na Japan katika sekta ya Miundombinu zikiwemo barabara nchini Tanzania, Mazungumzomyaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara,Jijini Dar es salaam.
 Ujumbe   kutoka Japani ukiongozwa na Balozi wa Japani Nchini Tanzania, Masaharu Yoshinda, ukisikiliza kwa Makini maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) kuhusu azma ya Tanzania kuwa na Bandari itakayo himili ushindani barani Afrika.
 Maafisa  kutoka Tanzania walioambatana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani), katika kikao na Balozi wa wa Japani Nchini Tanzania, Masaharu Yoshinda wakinukuu Maelezo yaliyokuwa yakitolewa, kuhusu umuhimu wa Miundombinu ikiwemo barabara na reli kwa manufaa ya watanzania, wakati walipokutana na kufanya mazungumzo Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake