Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa mkoa wa Kaskazini A, Unguja wakati wa Kufungua Mafunzo maalum ya Viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake wa ngazi ya Matawi, Wadi na Majimbo.
Wana CCM wa Kaskazini A wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mafunzo ya Uongozi yaliofunguliwa na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kaskazini A Unguja, Ndugu Juma Haji akihutubia kabla ya kumkaribisha Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua mafunzo maalum ya Uongozi yaliofanyika Mkokotoni Unguja kwenye Chuo cha Amali.
Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa CCM katika Mkoa
Kaskazini (A) Unguja kuwachukulia hatua stahiki wanachama ambao wanakisaliti na
kuhujumu shughuli katika hatua ya kujenga CCM mpya.
Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduz i(CCM) Taifa SAMIA SULUHU HASSAN ametoa kauli
hiyo wakati anafungua mafunzo maalum ya viongozi na watendaji wa CCM na Jumuiya
zake wapatao 556 katika ngazi ya matawi, wadi/tarafa na majimbo katika Mkoa wa
Kaskazini (A) Unguja.
Samia Suluhu
Hassan amesema kuwa hatua hiyo itasaidia chama kuimarisha shughuli zake kwa sababu
chama kitakuwa na watu waadilifu na wenye nia ya kukisaidia CCM kusonga mbele
na kupata ushindi mkubwa katika chaguzi zijazo.
Amesisitiza
wanachama na viongozi wa CCM kote nchini waendelee kuweka mipango na mikakati
imara itakayowezesha chama kuendelea kupata ushindi mkubwa na kushika dola.
Mjumbe huyo ambaye
pia ni Mlezi wa CCM katika mkoa wa Kaskazini A Unguja amesema Umoja na
Mshikamano miongoni mwa wananchama na viongozi ndio silaha madhubuti
itakayowezesha chama hicho kuimarisha shughuli zake na kuongeza maradufu idadi
ya wanachama nchini.
Amesema kwa sasa Viongozi watakiwa kujielekeza katika kufufua na kuimarisha jumuiya za chama ambazo katika baadhi ya maeneo hazifanyi kazi vizuri ili zianze kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia kanuni na taratibu za chama.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Taifa pia ameendelea kuonya baadhi ya viongozi waache tabia ya kutengeneza makundi ya ndani ya chama kwa ajili ya kusaka madaraka bali wawe mstari wa mbele katika kujenga umoja na mshikamano ndani ya chama.
Kuhusu mafunzo, Samia Suluhu Hassan amewahimiza viongozi wanaopata mafunzo hayo kuyatumia vizuri ili kuhakikisha wanaporudi kwenye maeneo yao wanafanya kazi kwa bidii na kwa uaminifu mkubwa.
Amesema kwa sababu Serikali iliyopo madarakani inatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi ni muhimu kwa viongozi wa chama katika ngazi zote washirikiane na viongozi wa Serikali katika maeneo husika ili kuhakikisha miradi ya maendeleo ya wananchi inafanyika kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake