Advertisements

Wednesday, January 11, 2017

Mtatiro amuomba rais kuokoa fedha za ruzuku za CUF


Mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya chama cha wananchi (CUF) Julius Mtatiro amemuomba Rais John Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Serikali kuchukua hatua za dharua kuokoa fedha za wananchi zilizochukulia na viuongozi wa upande wa pili wa chama hicho kama ruzuku kwa chama.
Mtatiro anasema, Viongozi wanaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba walichukua fedha kiasi cha Sh 369 na kuziweka katika akaunti ya chama wilaya ya Temeke kisha Akaunti binafsi tofauti na utaratibu sahihi ambao fedha zote za ruzuku huwekwa kwenye akaunti kuu ambayo inasimamiwa na Katibu mkuu wa Chama Maalim Seif.
"Januari 05 ambayo ilikua ni alhamisi ya wiki iliyopita akunti ya hazina ilishiriki katika utoroshaji wa fedha hizo ambazo baadae zilianza kugawanywa na kuhamishiwa katika akaunti binafsi chapu chapu kama zilivyochotwa pesa za Escrow," Mtatiro.

No comments: