Rais wa Jamhuri ya Uturuki, Mhe. Recep Tayyip Erdogan akiwa ameambana na mkewe Mama Emine Erdogan, wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Erdogan atakuwa nchini kwa ziara ya siku mbili kuanzia leo tarehe 22 Januari, 2017.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akimkaribisha Mhe. Rais Erdogan mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akisalimiana na Mhe. Rais Erdogan mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima akisalimiana na Mhe. Rais Erdogan mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, pembeni ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Ali Salum Hapi.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akisalimiana na Mhe. Rais Erdogan mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere.
Mhe. Rais Erdogan akisalimia sehemu ya vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitumbuiza uwanjani hapo wakati alipowasili.
Wakiendelea kutumbuiza.
No comments:
Post a Comment