MWANARIADHA Alphonce Simba ameipa Tanzania heshima kubwa baada ya kushinda mbio ndefu kwa wanaume (marathon) za msimu wa 14 huko Mumbai, India, zilizofanyika jana (Jumapili) ambapo alishika nafasi ya kwanza.
Wakati Tanzania ikifurahia ushindi huo, Kenya nayo ilifurahia ushindi wa nchi hiyo ambapo kwa upande wa wanawake ubingwa wa mbio hizo kwa upande wa wanawake ulibebwa na Bornes Kitur.
Simbu ambaye ni mwenyeji wa Mkoa wa Singida alihimili changamoto kubwa kutoka kwa mshindi wa pili Joshua Kipkorir wa Kenya ambaye alikuwa anamfuata nyuma kwa muda mrefu.
Wanariadha hao ambao hawakuwa wanaongoza mbio hizo katika dakika 90 za mwanzo, walijikuta wanatanguliwa na Kipkorir, mwanariadha ambaye alikuwa hajulikani. Baada ya saa moja na dakika 47 Simbu aliongeza kasi na kumfikia Kipkorir ambapo walikwenda bega kwa bega kwa dakika 20 hadi Simbu alipoongeza kasi na kumwacha Mkenya huyo.
Simbu alimaliza mbio hizo za kilimita 42.195 kwa muda wa saa 02 dakika 09 sekunde 32 ambapo Kipkorir alikuwa wa pili kwa muda wa saa 02 dakika 09 sekunde 50.
Lilikuwa pambano gumu… ulikuwa mtihani mkali,” alisema Simbu, baada ya mchuano huyo ambapo katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016 huko Rio de Janeiro alishiriki na kutopata ushindi akisisitiza wakati huu alikuwa amefanya matayarisho ya kutosha.
Kipkorir naye alishukuru kumaliza mbio hizo kwa ushindi huo akifuatiwa na raia mwenzake, Eliud Barngetuny.
Kitur ashinda marathon ya wanawake
MWANARIADHA wa kike, Bornes Kitur, aliipa heshima nchi yake ya Kenya kwa kuwa mshindi wa kwanza katika mbio ndefu za marathon ambapo alitumia saa 02 dakika 29 sekunde 02, akiwa mbela ya wanariadha wawili wa Ethiopia, Chaltu Tafa (aliyetumia muda wa 02:33.03) na Tigist Girma (02:33.19), waliomaliza wa pili na wa tatu kwa mfuatano.
Wanariadha hao, licha ya ushindi huo walikiri kwamba hali ya hewa haikuwa nzuri kwao katika sehemu ya milima mingi.
Ushindi wa wanaume na muda waliotumia
1 Alphonce Simbu (TANZANIA) 02:09.32
2 Joshua Kipkorir (KENYA) 02:09.50
3 Eliud Barngetuny (KENYA) 02:10.39
Ushindi wa wanawake na muda waliotumia
1 Bornes Kitur (KENYA) 02:29.02
2 Chaltu Tafa (ETHIOPIA) 02:33.03
3 Tigist Girma (ETHIOPIA) 02:33.19
Naomba Mr Simba ashiriki Boston Marathon ya mwezi wa nne hapa USA, atakuwa ametuletea heshima ya nchi pia, tunampongeza sana kwa kupeperusha bendera ya Tanzania.
ReplyDelete