Ni jambo la
kusisimua kutokana na huruka za vijana kwenye mitandao ya kijamii, hii ni mara
baada ya kuona matumizi mabaya ya mitandao kama Facebook,Twitter, Instagram nk
vikiongezeka. Vijana wengi wanashindwa
kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya
masilahi yao badala yake wamekuwa wakitumia mitandao hiyo, kutafuta wapenzi,utapeli,
umbeya, kuanika nyeti zao yaani kuweka picha chafu nk.
Katika video hii Kijana Moses alipata urafiki na msichana
ambaye anaitwa “Zaydar” mtandaoni, moses alivutiwa zaidi baada ya kuona picha
za mrembo Zaydar kwenye Instagram na ndipo alizidi kukoleza urafiki, kuomba
namba na kumtaka awe mpenzi wake, Zaydar hakukataa kwani na yeye alikuwa anatafuta mwanaume wa kumchuna
kisawaswa.
Picha alizo kuwa akipost
‘Zaydar’ kwenye mitandao yake ya kijamii hazikuwa zake, alikuwa anaweka picha
za warembo wengine ambao ni wazuri zaidi. Hivyo huruka ya moses alijua kuwa
msichana anaye wasiliana naye ndiye yule kwenye picha kumbe sio. Timbwili zito
ni badaa ya Moses na Zaydar kupanga (apointment) ya kuonana live Dar es salaam
– Buguruni – Sokoni … angalia video .. tunaomba Support sanaa ya Tanzania
Asante Tunamengi ya kukuelimisha kila wiki.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake