ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 30, 2017

ZAIDI YA WATU MILIONI MOJA WAMESAINI BARUA YA KUMZUIA RAIS TRUMP KURURU UINGEREZA

Haki miliki ya picha
Waziri Mkuu Teresa May alitangaza muwaliko huo wakati akiwa ziarani Marekani.

Zaidi ya watu milioni moja wa Uingereza wamesaini barua ya kutoa shinikizo kwa serikali ya Uingereza kusitisha ziara rasmi iliopangwa baadaye mwaka huu ya rais Donald Trump.

Barua hiyo iliyoandikwa kufuatia agizo la rais Trump dhidi ya wahamiaji, inaeleza kuwa kuja kwake kutamuaibisha Malkia Elizabeth.

Idadi ya watu wanaoendelea kusaini kupinga Mwaliko wa Trump nchini Uingereza inaendelea kuongezeka, tangu Marekani kuweka vikwazo dhidi ya wageni hatua iliyozua ghadhabu kote duniani. Amri ya Trump: Ni nani anaathirika?
Sudan yapinga amri ya Trump
Amri ya Trump: Ni nani anaathirika?


Waziri Mkuu Teresa May alitangaza muwaliko huo wakati akiwa ziarani Marekani.

Afisi yake imesema japo haikubaliani na baadhi ya sera za Trump hata hivyo ni vyema Uingereza kuwa na ushirikiano wa karibu na Marekani.

Kiongozi wa Upinzani Jeremy Corbyin ametaka Waziri Mkuu kuahirisha ziara hiyo.

Wengi wanaopinga wanasema ziara ya Trump nchini Uingereza itakua aibu kwa Ufalme.

Ziara rasmi za serikali Uingereza huambatana na mualiko kutoka kwa Malikia, ambae huwapokea viongozi wawili wa nchi kila mwaka.

Aiki jana Rais Trump aliweka sheria kusitisha mpango wa kuwapokea wakimbizi na hasa kuwapiga marufuku wakimbizi wote kutoka Syria na wengine kutoka nchi saba zote zikiwa za kiisilamu.
Jaji apiga marufuku amri ya Trump kurudisha wahamiaji makwao

Siyo mara ya kwanza kumekua na kampeini kumpiga Trump Uingereza.

Mwaka wa 2015 raia laki tano walisaini kutaka kiongozi huyo kupigwa marufuku Uingereza.

Kiongozi wa zamani wa chama cha Labour Ed Millibard amesema yeye na mbunge mwenzake ambae ni mzaliwa na Iraq Nadhim Zahawi wataitisha muswada wa dharura bungeni kujadili maombi ya raia.
Alex Salmond ambe alikua kiongozi wa Scotland amesema Trump hafai kupata muwaliko Uingereza, kauli yake ikiungwa mkono na Meya wa jiji la London Sadiq Khan

No comments: