ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 9, 2017

CHUO CHA DIPLOMASIA CHAPOKEA UFADHILI WA KOMPYUTA 150 KUTOKA KWA SERIKALI YA KOREA

Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia Mhe. Balozi Ombeni Sefue (wa pili kushoto) akipokea kompyuta kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Song Geum Young, wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia Dkt. Bernard Archiula. 
Mhe. Balozi Sefue akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Bodi na Uongozi wa Chuo cha Diplomasia mara baada ya kupokea ufadhili huo kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya Korea. 
Balozi Mwinyi akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo aliipongeza Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kuendelea kuwa mdau wa maendeleo katika sekta mbalimbali nchini hususan sekta ya Elimu. 
Sehemu ya Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia wakimsikiliza Balozi Sefue (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa neno la shukrani. 
Sehemu nyingine ya watumishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakishuhudia makabidhiano. 
Dkt. Bernard Archiula (wa kwanza kushoto), akifafanua jambo kwa Balozi Sefue na Balozi Mwinyi. 
Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga
Wakiwa katika picha ya pamoja. 

No comments: