ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 17, 2017

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA- MERERANI

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro wakati  aliposimama  akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani Februari 16, 2017.
 Mwananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro  akiwasilisha kero yake kwa njia ya bango akidai mawasiliano ya simu za mkononi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  aliposimama na kuwasalimia wananchi wa kijiji hicho waliokusanyika  barabarani. Alikuwa akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani Februari 16, 2017.
  Wananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aliposimama na kuwasalimia akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani Februari 16, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Mererani mkoani Manyara wakati alipowasili kwenye  eneo la mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa mikutano, Februari 16, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye  uwanja wa mikutano wa  Mererani mkoani Manyara, Februari 16, 2017.
 Baadhi ya wananchi  Mererani mkoani Manyara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia  katika mkutano wa hadhara  kwenye uwanja wa mikutano wa Mererani ,  Februari 16, 2017.
 aziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wingi wa mabango  katika mikutano ya hadhara  ya viongozi wakuu ni ishara ya wazi kuwa  watendaji wa  Halmashauri  hawawatembelei  wananchi na kutatua kero zao.
 Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mikutano wa  Mererani mkoani Manyara Februari 16, 2017, Mheshimiwa Majaliwa alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro na watendaji wake kukusanya mabango  yaliyokuwa yakionyeshwa na wananchi kwani mengi ya matatizo yanapaswa kumalizwa na viongozi hao  na aliwaagiza  kurejea Mererani siku inayofuata ili waitishe mkutano na  kujibu bango moja baada ya jingine.
Pichani,  watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wakikusanya mabango hayo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Ndugu Ali Juma baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara  kwenye uwanja mikutano  wa Mererani mkoani Manyara Februari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

1 comment:

Anonymous said...

Ndugu Viongozi wetu mlioteuliwa na mliochaguliwa. Yanayoonekana katika uongozi huu tulionao huenda ikawa kujirudisha nyuma kwa asilimia 70 ukidhania tumepata uhuru miaka miwili iliyopita hivyo tunaijenga nchi.! Nasema hivyo kwa machache tu
1. Viongozi waliochaguliwa na wananchi hawana jinsi wanavyoweza kujadiliana na waliowachagua kuleta maendeleo kutokana na walioteuliwa kuwa juu!
2. Maeneo.menginebyamekuwa na hata wapinzani ndio.kabisa wanaswekwa ndani na vifungo visivyokuwa na haki hawana mamlaka na mapendekezo endelevu. Wanazuliwa jambo kuwekwa ndani na baad ya siku waliochaguliwa wanaapata mwanya wa kupitia kwenye maeneo yao na kutoa vitisho.
3. Wananchi katika maeneo mengi hasa ya vijijini wana shida nyingi sana ambazo ziliahidiwa nyakati za kampeni na pia kuahidiwa mil. 50 kwa kila kijiji nako kumeleta shida hakuna mchango wowote wa kimaendeleo na fedha za halmashauri zinakoelekezwa ni serikali kuu! Ubunifu hakuna na ukijifanya kujua unatumbuliwa na mkuu wa mkoa au wilaya!
4. Kuna umuhimu sana wa kuwa na katiba timilifu na wale wote wanaoteuliwa na Rais wawe wanapitishwa na bunge kama wanafaa badala ya kuteuliwa leo na kesho kuapishwa! Wanaochaguliwa na wananchi wawahudumie wananchi wao ipasavyo bila kuingiliwa na ripoti zao ziende kwa mkuu wa Wilaya na hatimae Mkoa utakaolifikisha Serikali kuu.
5. Mkuu wa nchi apunguze kugawa fedha kienyeji na atumie wizara husika au bunge linalopanga bajeti.
Kutumbua tumbua hakutaendeleza nchi.
Sasa huvi serikalimimeacha kujali yale yaliyoahidiwa na tunaelekea kukabana na watumia viroba naa watengenezaji. Je kodi itakusanywaje? Je viwanda vya jirani navyo vimezuiwa kutengeneza??
Salaa.