ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 9, 2017

NDUGU WAGOMA KUCHUKUA MAITI ILIYOFIA MAHABUSU WAKISUBIRI MAJIBU KUTOKA KWA SIRRO

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
By Tumaini Msowoya, Mwananchi

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro leo anatarajia kutoa taarifa kuhusu tukio la kifo cha Petro Yakobo anayedaiwa kufa akiwa mahabusu katika Kituo cha Polisi Mbezi kwa Yusufu.

Yakobo ambaye ni mkazi wa Kibo jijini Dar es Salaam, ndugu zake wamegoma kuchukua mwili wake wakiwatuhumu polisi kumsababishia mauti. Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Dada wa marehemu, Happy Mhagama amesema hawatachukua mwili huo mpaka watakapojua sababu za kifo chake ili waweze kuchukua hatua za kisheria kwa sababu ndugu yao alipokamatwa alifika kituoni hapo akiwa mzima akisindikizwa na mkewe, Selina Yakobo kisha aliwekwa mahabusu.

Happy amesema siku iliyofuata, Selina alipompelekea mumewe chai alishangazwa kuambiwa amelazwa katika Hospitali ya Tumbi Kibaha akipatiwa matibabu kutokana na majeraha aliyopata baada ya wananchi wenye hasira kumpiga.

“Ndugu yetu alikuwa mzima wa afya wakati anakwenda polisi, hao wananchi wenye hasira walimpiga akiwa wapi?” amehoji Happy.

Tayari Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeingilia kati na sasa kinasubiri majibu ili kichukue hatua za kisheria kupitia kwa mwanasheria wake, Godfrey Mpandikizi.

No comments: