Mambo yalikuwa ni mazuri sana ndani ya King Solomoni Hall, usiku wa 11/2/2017 lilikuwa ni tukio zito tena lenye furaha na faraja kwa wadau mbalimbali wa mitindo hapa Tanzania. Lady In Red 2017 imekuwa ya kipekee zaidi baada ya wadau wengi kuitikia wito. Kwenye hiyo, Fashion Show wabunifu walioshiriki usiku huo walionekana kufanya vizuri zaidi.
Kwa upande wa Wabunifu ukweli walijipanga na kila mmoja alijaribu kutumia ujuzi wake katika kubuni kazi nzuri, hata wale upcoming Designers, walijitahidi kuandaa mavazi mazuri kiasi kwamba ilikuwa ni ngumu kujua nani upcoming na nani ni mzoefu katika Tasnia hiyo, hongera yao. Red carpet ili ng'ara na ku-shine zaidi coz watu walijipatia picha nzuri za kumbukumbu, bila kusahau interviews kutoka kwenye media tofauti tofauti za hapa Bongo.
Kumbuka Show hii huandaliwa na Mama wa Mitindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin, akishirikiana na wabunifu wengine. Katika Show hiyo walikuwepo designer wengi + models kama Martin Kadinda,Rukia Walele, Agusta Masaki, Kulwa Mkwandule, Ally Remtula, James Maunda, Paulina Mgeni, Omary Rashidi, Agness Bwagilo, Kasikana, na wengine kibao.
Hivyo ndivyo mambo yalivyo kuwa Tazama picha za tukio hapa
by Victor Petro.
No comments:
Post a Comment