ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 20, 2017

RAPPER METTY MUBASHARANI NA DAYNA NYANGE KWENYE KWENYE WIMBO WA YOUR LOVE

Rapper Metty kutoka jijini Dar es salaam ametangaza kachia kibao kipya kinachoenda kwa jina la YOUR LOVE.

Wimbo huo wenye mahadhi ya muziki wa kizazi kipya " bongoflava" maudhui yalioambatana kuimba na kurap kiasi mtindo unaowavutia mashabiki wengi wa muziki huo.

Katika wimbo huo Metty amemshirikisha mwanadada Dayna Nyange anaefanya vizuri kwenye medani ya muziki kwa sasa pamoja na muimbaji mwingine anaechipukia kwa kasi aitwae Nappy.

Wimbo wa YOUR LOVE umetengenezwa na mtayarishaji maarufu nchini Tanzania Mr T Touch katika studio za Touchez Sound zilizopo sinza jijini Dar es salaam.

Katika mahojjiano na mwandishi wa habari hizi Metty amesema wapenzi wa muziki wakae mkao wakupkea muziki mzuri wa level ya kimataifa,amejipanga vyakutosha na hivi punde ataachia kibao hiko ambacho kitapatikana katika vyanzo mbalimbali ikiwemo redio,lunimga na mitandao ya kijamii.

No comments: