ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 22, 2017

Waziri Mahiga apokea ujumbe wa Mhe. Rais kutoka kwa Mfalme wa Qatar


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea ujumbe wa Mfalme wa Qatar, Mtukufu Sheikh Tamim Hamad Bin Khalifa Al-Thani kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Ujumbe huo uliwasilishwa leo katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam na Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Abdullah Jassim Al Maadadi.

Waziri Mahiga akizungumza na Mhe. Jassim Al Maadadi ambapo pamoja na kuzungumzia masuala ya ushirikiano Waziri alimpongeza kwa hatua nzuri za maandalizi ya Kombe la Dunia linalotarajiwa kufanyika nchini Qatar mwaka 2022. Vilevile alimuarifu kuhusu hatua iliyofikiwa na Serikali ya Tanzania katika kukamilisha ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi mjini Doha, Qatar.

Mhe. Jassim Al Maadadi alitumia fursa hiyo kuwasisitiza Watanzania kuzichangamkia fursa za ajira zilizopo nchini Qatar wakati huu wa maandalizi ya Kombe la Dunia kwa kuwa nchi hizi zilikwisha saini mkataba wa ushirikiano kwenye kazi na ajira mwaka 2013.

Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga, Afisa Mambo ya Nje, Bw. Hangi Mgaka na Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu wakifuatilia mazungumzo.

Mazungumzo yakiendelea

Picha ya pamoja.

No comments: