Na WAANDISHI WETU| GAZETI LA AMANI| HABARI NA GPL
DAR ES SALAAM: Msanii wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuhusu kuachana rasmi na mpenzi wake ambaye ni msanii wa muziki kutoka Kundi la Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Rajabu Ibrahim ‘Harmonize’.
Akizungumza na mwandishi wetu jana, Wolper alikiri kwamba, yeye na Harmonize, mapenzi yao yamekwisha kabisa.
“Yah! Ni kweli, nimeamua tu kuachana naye. Unajua katika uhusiano kuna kugombana, tumekoseana na kusameheana mara nyingi, sasa tumeamua kila mtu aendelee na maisha yake. Kwangu ni fursa nzuri kwani nitakuwa na amani ya moyo. Maisha yatasonga na nitajikipu ‘bize’ na kazi zangu. “Siwezi kujutia uamuzi huu na moyo wangu umeshazoea, kanikuta nikiwa Wolper na tumeachana nikiwa Wolper labda kama angekuwa amenikuta Fatuma na kunifanya kuwa Wolper.
“Harmonize nimedumu naye kwenye mapenzi kwa mwaka mmoja tu. Nilimkosea, akanikosea kanikosea tena, siwezi kuongelea kitu halisi alichonikosea lakini jua hilo.
“Wakati tukiwa kwenye uhusiano wetu hatujawahi kuchiti (kusaliti) au inawezekana tulichiti na tukasameheana ila kwangu ni rahisi kusamehe kwa kuchiti kuliko kukusamehe kwenye kosa dogo ambalo wewe unaliona ni la kawaida lakini kwangu nikahisi kama unanishusha thamani, na ninapoingia kwenye uhusiano huwa nasema vitu ambavyo sivipendi kukosewa, na nikiona unakosea mara kwa mara najua hiyo ndiyo tabia yako,” alisema Wolper na kuongeza:
“Hata sikumbuki mara ya mwisho niliongea naye lini ila neno lake la mwisho kwangu lilikuwa ni samahani ambalo sijalikubali.” Juhudi za kumpata Harmonize zinaendelea baada ya jana kutokupatikana hewani.
No comments:
Post a Comment