Makamu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho kuwateuwa Lawrence Masha na Ezekia Wenje kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki pamoja na mambo mbalimbali yayoendelea nchini. Kulia ni Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtaka Rais Dk. John Magufuli kuueleza umma wa Watanzania sababu za kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
Katika hatua nyingine kimesema wabunge wa vyama pinzani kwa kushirikiana na wabunge wa Chama cha Mapinduzi wanatarajia kuwasha moto katika Bunge la Bajeti linalo tarajia kuanza mapema mwezi ujao kulingana na mambo mbalimbali yautendaji wa Serikali ya awamu ya tano.
Aidha chama hicho kimemtaka Rais Magufuli kumchukulia hatua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutii matakwa ya wananchi na kuepuka hali ya kuonekana kutumia vibaya madaraka kwa kuwahukumu baadhi ya watu kwa kuwalinda watu wenye makosa ya wazi wazi.
Akizungumza Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam leo siku moja baada ya kutenguliwa kwa uteuzi huo Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Chadema Bara, John Mnyika alisema kutokana na taarifa ya Ikulu kutoeleza sababu za kutenguliwa kwa nafasi ya Nape hivyo ipo haja kwa Rais kueleeza wazi sababu ya kumuondoa.
"Rais anapaswa kujitokeza kutoa sababu kwanini katika kipindi hichi ambacho kamati iliyoundwa na Waziri kutoa taarifa iliyoeleza wazo makosa yaliyofanywa na Makonda katika siku chache baada ya Rais kumkingia kifua," alisema.
Alifafanua kuwa hatua ya Rais Mgufuli kumuondoa Nape ni matumizi mabaya na ya wazi ya madaraka katika kuwahukumu baadhi ya watu na kuwalinda watu ambao wanafanya makosa ya wazi wazi.
"Chimbuko la matatizo haya ni Mkuu wa Mkoa huo na kauli za Rais Magufuli katika kipindi cha siku za karibuni kuhusiana na Makonda kwa gharama yeyote ya kumlinda Makonda ni wazi kwamba ni matumizi mabaya madaraka," alisema.
Hata hivyo alisema kuwa matumizi hayo mabaya ya madaraka kwa sasa yamejipenyeza zaidi hali ambayo kwa sasa hayamuhusu Rais Pekeake bali hata watendaji wa vyombo vya dola ambavyo pia vimejidhihirisha kutokana na matukio yanayoendelea ikiwemo matumizi ya silaha kwenye maeneo ambayo hayakuhitajika.
Alisema ipo haja kwa Rais Magufuli kuwaeleza watanzania kuhusiana na baadhi ya maofisa wa ulinzi na usalama waliovamia kituo cha Luninga cha Clouds wakiwa na silaha na walio mtishia bastola Nape kama amewatuma na kama hakuwatuma pia aeleze hadi sasa ameelekeza wachukuliwe hatua gani, akiwa yeye ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.
Aidha alitumia nafasi hiyo kumpa pole kwa wanahabari na Nape kutokana na mambo mbalimbali yanayowakuta, na kuwataka Watanzania kutarajia kuwashwa moto katika Bunge la Bajeti linalotarajia kuanza hivi karibuni katika kujadili mambo mbalimbali yanayotokana na utendaji wa Serikali.
"Naamini safari hii hatutakuwa wabunge wa Chadema au wa vyama vya upinzani pekee bali naamini safari hii Bunge litakuwa kitu kimoja katika kuchukua hatua wakiwemo wabunge wa CCM," alisema.
Kuhusu wabunge walioteuliwa kushiriki katika uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, aliwataja walioteuliwa kutoka katika chama hicho kuwa ni Lawrence Macha na Ezekia Wenje.
Alibainisha kuwa wagombea hao walipatikana kutokana na vikao vya siku mbili vya Kamati Kuu ya Chadema vilivyo fanyika hivi Machi 22 na 23 mwaka huu.
3 comments:
Kwani wao chadema walishawahi kuwaeleza watanzania kwanini Zito Kabwe alifukuzwa kiuonevu chadema? Ndani ya uongozi wa nape zaidi ya shamra shamra nyingi lakini ndio wakati watanzania waneshuhudia maadili kwa vijana wao wa kitanzania yakiporomoka kwa kiasi kikubwa kabisa. Picha za ngono za vijana wa kitanzania kwenye mitandao ni vitu vya kawaida. Wakati wa Nape ndio kiwango cha mpira kwa level ya FIFA kwa timu ya taifa kimekuwa cha chini na cha aibu kuliko wakati wote. Kama vile haitoshi Nape amechangia na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuondosha mjadala wa vita zidi ya madawa ya kulevya. Na kama vile haitoshi tena, Nape alikuwa anachukua hatua ya kumuajibisha mkuu wa mkoa wa Daresalam bila ya kupitia ngazi husika ebo..Tanzania na serikali sio wizara ya habari peke yake.
Sikubaliani nawe anonymous wa 10:48 AM. Mimi ni mwana CCM, na kitendo cha kumfukuza Nape kina utata. Usimlinganishe Zitto na Nape. Kwa CCM, Nape alitoa mchango mkubwa sana katika kampeni zilizomweka JPM madarakani. Zitto hakufanya kampeni yakuiweka serikali ya JPM. Nina uhakika hata wewe ni beneficiary wa jasho ambalo Nape na mamilioni ya vijana wa CCM walitokwa kumpatia kazi Rais Magufuli. Huyu Makonda naye ni beneficiary wa jasho la Nape na vijana wa CCM. Nina uhakika siyo wengi ambao wako kwenye baraza la Mawaziri, walitoka jasho kwenye kampeni. Contrary to your opinions, Nape deserves our gratitude and respect. Wabunge na Wanasiasa wengi wa CCM wanashukuru mchango mkubwa wa Nape kwa Chama na nchi with the exceptions of Makonda and a few haters like you anonymous @10:48 AM. One thing for sure is that, Nape is young, intelligent, and vibrant politician. He is a force to reckon with in Tanzania's political scene for many years to come. Asante mhe. Waziri Mwigulu kwa jitihada zako za kumsaka yule thug ambaye ameliabisha jeshi la polisi, na kuwafanya watoto zetu kujiuliza kama hii ndiyo Tanzania itakayowalea kwenye mitaa iliyobadilika ambako askari wanachomoa bastola kiholela holela kama the Wild-West ya maCowBoys.
yani wanachokifanya chadema ni sawa na mwenye nyumba anapo amua kumfukuza kazi house girl wake kisha wewe jiranai ambaye ulikuwa unanufaika na huyo house girl kwa namna unayoijua wewe uanze kuhoji na kumshutumu mwajiri huyo wa house girl kuwa ni kwanini kamfuta kazi mbaya zaidi ukatoa kabisa na muda wa kujibiwa hivyo viswali vyako hewa...sasa cha kujiuliza ni kwamba mambo yanayo fanyika nyumba ya jirani yanakuhusu nini?ndio maana chadema mnaitwa wachochezi na wachafuzi wa amani najuta kuwapigia kura mwaka jana
Post a Comment