| Bi. Agatha Nderitu akiwasilisha matokeo ya utafiti wa namna nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zilivyotekeleza Itifaki ya Soko la Pamoja kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2014 hadi 2016. Utafiti huo ulilenga maeneo ya Soko huru la bidhaa, mitaji na uhuru wa watu kusafiri ndani ya Jumuiya. Utafiti huo ulionesha kuwa nchi za EAC zimejitahidi kutekeleza Itifaki hiyo ingawa bado kuna vikwazo na sheria zinazozuia utekelezaji wa soko hilo kikamilifu hususan kwenye vikwazo visivyo vya kibiashara. |
No comments:
Post a Comment