Miss Tanzania 2004, Nargis Mohamed (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo nia yao ya kuanzisha darasa la urembo la kidigitali. Pembeni ni Mjasiliamali Nafue Nyange.
Miss Tanzania 2004, Nargis Mohamed.
Mjasiliamali Nafue Nyange.
Miss Tanzania 2004, Nargis Mohamed na Nafue Nyange wameamua kufungua shule ya urembo watakayokuwa wakiitoa kwa njia ya mtandao.
Wakizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Nargis alisema kuwa wameamua kuandaa mafunzo hayo maalum katika fani ya urembo ili kuweza kuwawezesha wananwake na vijana waweze kujikwamua kiuchumi.
Nargis aliongeza kuwa mafunzo hayo maalum yamewalenga watu wote na wanaweza kuyapata kidigitali zaidi ikiwemo njia ya simu au mtandao kwa gharama ya shilingi elfu kumi (10,000) tu za kitanzania kwa mwezi.
"Mafunzo hayo hayachagui jinsia; nia yetu kubwa sisi ni kuwawezesha wenzetu kwa kuwapa ujuzi ili waweze kujiinua kiuchumi kama wajasiliamali na kujijenga kimaisha sambamba na mpango wa serikali yetu kujenga ajira na kujikwamua kutoka kwenye umaskini," alisema Nargis.
Kwa upande wake Nafue Nyange aliongeza kuwa mafunzo hayo yanapatikana kwa bei nafuu kabisa kupitia tovuti ya www.glammadamlive.com, anawaomba watanzania wasajili wataweza kufanya malipo kupitia Vodacom M-pesa na Tigo Pesa. Kwa wale walio nje ya nchi wanaweza kutumia kadi tofauti kama VISA,MasterCard,American Express.
No comments:
Post a Comment